KOCHA wa timu ya ngumi ya Mkoa wa Kigoma
Juma Lesso amesema timu yake ya mkoa imekuja kamili kwa ajili ya
mashindano ya wazi yatakayofanyika Feb 5
katika viwanja vya Tanganyika Peckers vilivyopo kawe jijini Dar es salaam
Hii mara ya kwanza kwa timu ya Mkoa wa
Kigoma kushiriki mashindano makubwa kama haya na timu hiyo ambayo imeweka
kambi yake maeneo ya kawe kabla ya hapo ilikuwa maeneo ya mabibo na sasa
kawe kwani mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Feb mosi mwaka huu na
sasa yakisogezwa mbele hadi feb 5
Amekaririwa akisema
"Tunamshukulu sana Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya kwa kuhakikisha tunashiriki katika
mashindano haya kwa mara ya kwanza"
Timu hiyo ambayo imekuja na wachezaji
kumi kati ya hao wanawake watatu na wanaume saba ambao wakekuja
kuwakilisha mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuchukuwa ubingwa huo ambao upo wazi
Lesso ambaye ni kocha wa kimataifa wa
mchezo huo ambaye amepitia kozi ya kimataifa ya mchezo aliwataja baadhi ya mabondia aliokuja nao kuwa ni Agnes Mushi, Eliza
Josefu, Rashidi na Abasi na wengine ambao walikuwa katika kambi ya mkoa
huu wa Kigoma
No comments:
Post a Comment