Meneja mstaafu wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameeleza imani
kuwa miamba hao wa Uingereza watapata mwelekeo chini ya mrithi wake
David Moyes.
United wamezorota musimu huu huku Moyes akishindwa kuendeleza ufanisi uliokuwa kawaida chini ya Ferguson.
Mabingwa hao wa ligi ya Premier wamo nafasi ya saba kwenye jadwali
na wanakondolea kungolewa kutoka kombe kuu bara Uropa, Champions League,
baada ya kupoteza mkondo wa kwanza raundi ya mwondoano 2-0 dhidi ya
Olympiakos.
Wengi sasa wanataka United wastahimili hasara na kumtaliki Moyes
lakini Ferguson amemtetea raia mwezake wa Scotland aliyekuwa meneja wa
Everton akisema ana uwezo wa kuimarisha magwiji hao.
“Watakuwa sawa. Bado ni mapema na kumekuwa na mabadiliko mengi na
Moyes anastahili muda. Nilikuwa hapo miaka 27, kwa hivyo itamchukua
meneja mpya wakati,” Ferguson alisema.
Chini ya enzi yake, United walizoa mataji 26.
No comments:
Post a Comment