Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti kumbe aliwataka wachezaji wake kukabiliana na watukutu wa Atletico jana katika hali yoyote ili angalau kupata alama muhimu ambayo itaendelea kuwaweka katika usukanani wa ligi kuu ya Hispania La
Liga.
Bao la dakika za mwisho lililofungwa na Cristiano Ronaldo liliwaokoa Real Madrid angalau kupata sare ya mabao 2-2 katika mchezo mgumu maarufu kama 'Madrid derby' katika dimba la Vicente Calderon hapo jana Jumapili.
Matokeo hayo yana maanisha kuwa Real wako mbele kwa alama moja dhidi ya wapinzani wao wakubwa Barcelona.
"Wao [Atletico] walikuwa wanajaribu kucheza mchezo wa vurugu. Tulijaribu kucheza na hatimaye tukafanikiwa kupata sare" Amesema Ancelotti.
"Tuemepata sare katika mchezo ambao pengine tungepoteza.
Kocha msaidizi wa Atletico Madrid German Burgos akipozwa na kurejeshwa kutoka kwa mwamuzi ambapo alikuwa akimlalamikia mwamuzi wakati wa mchezo dhidi ya Real jana. |
"Uwajibikaji ulikuwa mzuri na mwisho wa yote tunaweza kuridhika kwasababu Atletico ni wazuri hususani wanapokuwa katika uwanja wa nyumbani
No comments:
Post a Comment