Mshambuliaji wa Olympiakos Michael Olaitan anaelezewa kuwa yuko katika hali nzuri katika hospitali moja ya nchini Ugiriki baada ya kupoteza fahamu katika kipindi cha kwanza cha mchezo walioambulia kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa wa jiji la Athens, Panathinaikos.
Mshambuliaji huyo raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 21, alikuwa akikimbia na mpira na kuanguka kabla ya kupoteza fahamu.
Mapema meneja wa Panathinaikos Yannis Anastasiou, kocha wa zamani wa Reading, alianguka chini baada ya kugongwa kitu kilicho rushwa kutoka kwa watazamaji.
Olaitan, ambaye aliisaidia Olympoakos kuichapa Manchester United ba 2-0 februari 25 kabla ya kupelekwa hospitali aliaanza kupata ahueni na kurejea katika fahamu ambapo alifikishwa hospitali na kufanyiwa vipimo.
"Nina furaha kumthibitishia kila mmoja kuwa baada ya vipimo vya awali , hakuna dalili za hali kuwa mbaya" Amekaririwa mwakilishi wa Olaitan Paschalis Tountouris akisema..
"Kinachoonekana ni kuwa Michael alikuwa na matatizo ya 'viral myocarditis-Myocarditis is a heart condition caused by a virus, such as rubella, Epstein-Barr, and adenovirus.
Sasa kwa tahadhari ni kwamba Michael atasalia hospitali kabla ya kufanyiwa vipomo zaidi siku chache zijazo"
Mchezo ulikuwa bila ya kufungana wakati Olaitan akianguka na kupoteza fahamu.
No comments:
Post a Comment