Meneja wa Newcastle Alan Pardew amekutwa na tuhuma za kujibu kwa chama cha soka cha England FA kutokana na kukabiliana na kiungo wa Hull City David
Meyler kwa kumsugua kwa kichwa.
Hata hivyo imethibitika kuwa bosi huyo wa Magpies ameonekana kuwa hana hatia ya kujibu polisi kwani hakukuwa na shitaka lolote liliwasilishwa polisi dhidi yake.
Taarifa ya FA imesema
‘Meneja wa Newcastle United Alan Pardew
amedhiwa kufuatia kuhusiana na tukio la mchezo baina ya timu yake dhidi ya Hull City Machi mosi 2014.
‘Anatuhumiwa kwamba kunako dakika ya 72 ya mchezo huo Pardew alihusika katika tukio lililo mkutanisha na mchezaji wa jamabo ambalo ni makosa.
Pardew amepewa mpaka Alhamisi saa 12 jioni kujibu shitaka hilo’
Polisi wa eneo la Humberside wamethibitisha kuwa hawajapokea lalamiko kutoka kwa Meyler
klabu yenyewe na wanafurahia kuwa yatosha kwa FA kushughulikia suala hilo.
Inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo Rich Kirven amenukuliwa akisema
‘Tumefanya kazi ya pamoja na FA kwa kushirikiana na klabu yenyewe na kwamba wataendelea nalo barabara.
Pardew alitolewa na mwamuzi wa mchezo huo Kevin Friend mpaka jukwaani baada ya kukabiliana na Meyler kwa kugongana na mchezaji huyo wakati akiukimbilia mpira katika mstari wa pembeni wa uwanja katika mchezo wa ushindi kwa Newcastle wa mabao 4-1 mchezo uliopigwa KC Stadium Jumamosi.
No comments:
Post a Comment