KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 26, 2014

Mlinzi wa Arsenal Bacary Sagna awatolea nje Inter Milan

Mlinzi wa Arsenal Bacary Sagna ameamua kusalia England, hii ni kwa mujibu wa Rais wa Inter Milan Erick Thohir.

Kiongozi huyo wa juu wa klabu hiyo kongwe nchini Italia mapema wiki hii ametabaisha kuwa Inter ilikuwa katika mazungumzo na mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31 juu ya uwezekano wa kuanza kutoa huduma ndani ya San Siro msimu ujao, mkataba wa mchezaji unatarajiwa kumalizika majira ya kiangazi.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo hii leo Thohir amedhihirisha kuwa Sagna amegomea mpango huyo wa Inter kuweza kujiunga nayo.

‘Nadhani Bacary Sagna hatawasili kwasababu ameamua kusalia katika Premier League,’ Thohir alikuwa akiongea na wanahabari katika uwanja wa ndege wa Milan.

Sagna kwasasa yuko katika mazungumzo na Arsenal juu ya kuongeza mkataba wake ndani ya Emirates lakini Manchester City, ambayo walichukua wachezaji wawili kutoka Arsenal Samir Nasri na Gael Clichy, wamekuwa wakihusishwa kuwa na mapango na mlinzi huyo.

Thohir pia ametanabaisha kuwa klabu yake ya Inter haina mawasiliano na mlinzi wa kushoto wa Manchester United Patrice Evra, ambaye huenda akaondoka Old Trafford wakati wa  kiangazi.

‘(Patrice) Evra? We have had no contact for him,’ he added.

No comments:

Post a Comment