KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 26, 2014

ARSENE WENGER: UBINGWA SASA BASI TUJIAHADHARI NA KUKOSA NAFASI YA KLABU BINGWA ULAYA

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ni kama amekiri kwamba hawawezi kushinda ligi na ameonya kuwa sasa wanalazimika kuangazia kumaliza katika nne bora baada ya kulazimishiwa sare ya 2-2 nyumbani na Swansea City kwenye Ligi ya Premia hapo jana Jumanne.

Vijana hao wa Wenger walianza wiki moja iliyopita wakiwa miongoni mwa wanaopigania taji lakini wameteleza baada ya kutwangwa 6-0 na viongozi Chelsea katika mechi ya 1000 ya Wenger tangu kuanza kuitumikia timu hiyo, ambapo sare dhidi ya Swansea iliyotokana na bao la kujifunga dakika za mwisho lake Mathieu Flamini.

Arsenal sasa wako alama sita mbele ya Everton walio katika nafasi ya tano, ambao waliilaza Newcastle 3-0 Jumanne na wana mechi ambayo hawajacheza, huku wakipigania nafasi ya kushiriki Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

"Kushinda taji si hofu kubwa kwetu sasa,” Wenger aliambia kikao cha wanahabari.
“Lazima tuongee ukweli. Lazima sasa tutazame nyuma yetu. Everton walishinda, na bila shaka, sasa lazima tungazie mechi yetu ijayo (nyumbani dhidi ya Manchester City).

"Manchester City walipata matokeo mazuri usiku wa jana (ushindi wa 3-0 dhidi ya Manchester United). Wanaonekana kuwa moto. Wao na Chelsea ndio wanaopigiwa upatu sasa kushinda taji.

 Hatuna nafasi sasa ya kurudi mbioni.
Chelsea wana alama 69 kutoka kwa mechi 31 mbele ya City walio na alama 66 kutoka kwa mechi 29, huku Liverpool wakiwa nambari tatu na alama 65 kutoka mechi 30, Arsenal wa nne na alama 63 kutoka mechi 31 nao Everton alama 57 kutoka kwa mechi 30.

Nafasi ya Arsenal eneo la kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya inaonekana kuwa hatarini zaidi ikizingatiwa kwamba Manchester City watatua The Emirates Jumamosi kabla ya vijana hao wa Wenger kwenda Everton Aprili 6.
"Matokeo hayo yanavunja moyo,” alisema Wenger. “Tukiwa 2-1 labda tuliogopa sana kwa sababu kujiamini kwetu kuliathiriwa na matokeo ya Jumamosi na tulitaka kushinda tu mechi bila kujitokeza sana na kushambulia.”
"Kosa lilitendeka na likapelekea matokeo ambayo hatukutana usiku huu.”

No comments:

Post a Comment