Kikosi
cha Taifa Stars kimeondoka leo alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa ajili ya
mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya
wenyeji itakayochezwa Machi 5 mwaka huu.
Taarifa ya shirikisho la soka nchini TFF imesema Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu 25 unaoongozwa
na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu imefikia hoteli ya Safari jijini humo.
Mechi
hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars kipo
chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya
ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Namibia
(Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia kambini jana
(Machi 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi zake zilianza kuuzwa
Februari 28 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment