KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 1, 2014

Wenger ashambulia wakosoaji wa Arsenal

Arsene Wenger amesema “hahitaji kutetea” uamuzi wake wa kuwapa wachezaji wa Arsenal siku mbili za mapumziko wiki hii na kushambulia ukosoaji “wa kushangaza” ambao hatua hiyo imeibua.
“Si lazima iwe ni uchovu, sioni ni kwa nini hili ghafla limekuwa tatizo,” Wenger alisema Alhamisi. “Tumecheza bila kupumzika tangu Desemba, si lazima tueleze sababu, ni jambo la kushangaza.
“Tuko katika jamii ambalo kila mmoja anataka kudhibiti kila kitu; sielewi hili hata kidogo.
“Tuna haki ya kufanya mambo yasiyo ya kawaida. Tumetoka kucheza kipindi cha mechi ngumu. Tulichukua siku mbili za kupumzika, ni hayo tu.
“Wakati mwingine huwa si mwili tu, pia akili, unakabiliwa na presha kila wakati, hakuna jambo la ajabu hapa,” Mfaransa huyo alieleza.
“Wakati mwingine unapokabiliwa na presha ya aina hii, ni vyema kupumzika.
“Kazi yangu ni kutoa timu bora zaidi ambayo inaweza kushinda mechi, na si kuhusu watu binafsi, ni kuhusu timu.”
Hayo yakijiri, Wenger aliongeza kuwa anatarajia Mesut Ozil aweza sawa kucheza pale wapiganiaji hao wa taji la Ligi ya Premia watakapozuru Stoke Jumamosi.
Na alisema anatarajia Ozil aweze kusahau masikitiko ya kukosa penalti wakati wa kichapo cha 2-0 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mikononi mwa Bayern Munich wiki iliyopita.
"Yeye (Ozil) alikuwa na mechi ngumu kwa sababu alikosa penalti, na hilo likamwingia akilini,” akasema Wenger.
Mchezaji wa Arsenal ambaye amefana sana Ulaya majuzi, ingawa si akichezea klabu hiyo ya London, ni Joel Campbell.
Yuko Olympiakos kwa mkopo na alifunga bao safi timu hiyo ya Ugiriki iliposhinda 2-0 dhidi ya Manchester United mjini Piraeus Jumanne.
“Alicheza vyema sana (Manchester United), akishambulia, anaonekana kana kwamba amezoea uchezaji wa kutumia nguvu Ulaya,” akasema Wenger.
"Tulijua kwamba alikuwa na kipaji cha kufanya mambo mazuri.
“Alitegemea sana hayo, lakini sasa amechezea katika klabu tatu tofauti; Lorient, Sevilla, na Betis.
"Sasa yuko Olympiakos na amejifunza ukali wa ligi za Ulaya.
"Nitaamua (kuhusu maisha yake ya usoni) baadaye, lakini mbona isiwe? Tulimnunua kumleta hapa.”

No comments:

Post a Comment