Mechi
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka nchini Tanzania TFF ni kwamba mapato
hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo
kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga
ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna
sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja
sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh.
33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
Nayo
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa
jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata
mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni
sh. 3,143,898.31.
No comments:
Post a Comment