Mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney amesema
kuwa kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa Liverpool ni kama
janga kwake na hiki ndio kipindi kigumu kwake kuwahi kukishuhudia tangu
kuanza kucheza soka ya kulipwa.
Steven Gerrard aliingiza mabao mawili kutokana
na mikwaju miwili ya Penalti na kukosa la tatu kabla ya Luis Suarez
kuongeza bao la tatu.
Mchezaji Nemanja Vidic alifurushwa uwanjani kwa kufanya masihara.
Rooney mzaliwa wa Liverpool mwenye umri wa miaka
28, amesema kuwa hiki ni kipindi kigumu sana kwake na wembe ambao
hautoshi hata kumezwa.
"hili ni jinamizi . Ni siku mbaya sana kwangu , sijawahi kuhisi vibaya hivi maishani mwangu nikicheza soka.
''Yaani hata ni vigumu kutafakari. Liverpool ilicheza vyema sana , lakini hii ni hali ngumu kwangu, '' alisema Rooney
''Hakuna anayetaka kushindwa hapa hasa katika uwanja wa nyumbani, sio vizuri.''
Rooney,aliyesaini mkataba mpya na klabu hiyo,
mwezi jana , alipata tu fursa moja ya kujaribu kuingiza bao katika mechi
hiyo ambayo Liverpool ilidhibiti tangu mwanzoni ingawa hakufanikiwa
Man U wanashikilia nafasi ya saba katika jedwali
la pointi , ingawa Rooney anayepokea mshahara wa pauni laki tatu kwa
wiki amesema kuwa hajafa moyo sana kutokana na matokeo mabaya ya
Manchester United.
Kocha wa klabu hiyo David Moyes amesema kuwa aliachwa kinywa wazi asijue la kusema.
No comments:
Post a Comment