Waendesha mashitaka wa Ujerumani wamesema hawatakata rufaa dhidi ya
kifungo cha miaka mitatu na nusu alichohukumiwa Uli Hoeness kwa
mashitaka ya kukwepa kulipa kodi.
Kumaanisha kuwa rais huyo wa zamani wa Bayern Munich anaweza sasa kuanza
kutumikia kifungo hicho gerezani.
Hoeness mwenye umri wa miaka 62, na
ambaye ni mmoja wa watu maarufu zaidi katika soka la Ujerumani,
alihukumiwa wiki iliyopita kwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha euro
milioni 28.5 kupitia yake ya benki ya Uswisi. Alisema kuwa hatokata
rufaa na akajiuzulu kama rais wa Bayern.
Hivyo basi anatarajiwa kuanza
kutumikia kifungo chake katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
Hoenness amepata mafanikio makubwa akiwa kama mchezaji na klabu hiyo ya
mjini Munich , ambapo alijiunga na klabu hiyo mwaka 1970, akishinda
vikombe vitatu vya ulaya. Lakini ni katika utendaji wake kama meneja
mkuu ambapo aliibadilisha Bayern Munich kuwa moja kati ya vilabu vikubwa
barani Ulaya.
Akikubali wadhifa mwaka 1979 akiwa na umri wa miaka 27 , muda
wake wa kucheza kandanda ukiwa umemalizika mapema kutokana na kuwa
majeruhi, Hoeness alitumia uwezo wake wa kibiashara na kampuni yake ya
kutengeneza nyama za soseji barani Ulaya kuleta wafadhili na vitega
uchumi katika muda wote wa uongozi wake wa miaka 31 katika klabu hiyo.
Katika maelezo aliyoyatoa katika kituo cha televisheni cha taifa ARD
mwenyekiti wa shirika linalopambana na rushwa duniani Transparency
International nchini Ujerumani Caspar von Hauenschild amesema viatu vya
Uli Hoenness ni ngumu kuvivaa wakati huu.
"Katika kila baraza la ushauri, mwenyekiti wa baraza hilo ndie mwenye
mamlaka makuu, katika shirika lolote lile. Wakati inapotakiwa kuchukua
maamuzi magumu sauti yake inakuwa nzito. Uzito wa sauti hii kwa Uli
Hoeness kwa mtazamo wangu si rahisi kwa kweli kuipata tena."
Hoennes alikuwa rais wa Bayern Munich mwaka 2010, na mafanikio
yaliendelea, kwa timu hiyo kushinda mataji matatu kwa msimu mmoja mwaka
jana 2013. Kile anachokiacha Hoeness kwa klabu hiyo ni kwamba kuondoka
kwa Hoennes itakuwa si rahisi lakini si kwanza haitawezekana kuiendeleza
hali hiyo ya mafanikio. Bidhaa ambayo ni Bayern Munich itaendelea
kuvutia soko duniani kote, wakati kikosi cha timu hiyo kina uwezo mkubwa
hivi sasa katika Bundesliga ambapo fedha zinazopatikana kutoka katika
kushiriki katika champions league hazitakatika. Herbert Hainer
aliteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa baraza la ushauri la Bayern Munich,
klabu hiyo imetangaza siku ya Ijumaa.
No comments:
Post a Comment