KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 26, 2014

Giggs anaelekea kukabiliana na Norwich akiwaomba mashabiki wa 'The Stretford End' kumuunga mkono

Ryan Giggs atakuwa akitarajia mpinzani wake wa leo Norwich City watamuhakikishia safari njema akiwa meneja wa Manchester United kwa muda kwa mara ya kwanza.
Giggs mwenye umri wa miaka 40, ameandika katika ukurasa wake mpya wa umeneja 'A word from the boss', karika kumbukumbu zake za furaha anakabiliana na The Canaries.

'Nina kumbukumbu kubwa za kucheza dhidi ya Norwich," ameandika Giggs.

'Mapema katika kazi yangu ya uchezaji nakumbuka msimu wa 1992/93 pale ambapo timu zote zilipokuwa zikishindana kushinda Premier League na tulishinda kule Carrow Road ushindi wa taji la kwanza la ligi katika kipindi cha miaka 26 .' 

'Nilikamilisha mchezo wangu wa 900 wa kuichezea United ndani ya Norfolk na nilifunga goli za dakika za mwisho katika mechi iliyokuwa ngumu. Sitasahau kadhia za mashabiki waliosafiri siku hiyo kwakweli huwezi kuamini kumaliza na wapinzani wagumu.’

Giggs anategemea upendo kutoka eneo maarufu la mashabiki wa klabu hiyo maarufu kama 'The Stretford End' akimini kuwa yeye ni chaguo sahihi la kurithi mikoba ya David Moyes kama meneja wa muda.

No comments:

Post a Comment