KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 26, 2014

MHOLANZI AKABIDHIWA MIKOBA TAIFA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka Uholanzi kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).
 Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu) kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akiwa amefuatana na Makamu wake Wallace Karia, amesema anafurahi kumtangaza Nooij na ana matarajio kuwa Tanzania itanufaika na uzoefu wake mkubwa wa ukocha, hasa katika bara la Afrika.
 “Nawaahidi Watanzania kuwa sitomuingilia kocha katika kazi yake. Kama mimi sitomuingilia kocha, basi hakuna mtu yeyote atakayemuingilia. Tumemwajiri yeye kwa vile ni mtaalamu, hivyo hakuna sababu ya kumuingilia,” amesema Rais Malinzi.
 Naye Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili amesema yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.
 Amesema kabla ya kukubalia kufundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia, lakini vilevile amewahi kufundisha mpira wa miguu barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.

 Wasifu wake
Nooij amewahi kuwa kuwa mkufunzi wa maendeleo katika chama cha soka nchini Uholanzi kabla ya kuanza kuafanya kazi katika kituo cha  EVC 1913 katika nchi za Marekani na Kazakhstan. Amekuwa pia meneja wa timu ya vijana ya Bukina Faso ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 katika fainali za kombe la dunia la vijana la Fifa mwaka 2003.
Mwaka 2004 alikuwa ni kocha msaidizi wa klabu ya FC Volendam ya nchini Uholanzi.
Mwka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Msumbiji na akiwa kama meneja aliiwezesha nchi hiyo kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2010 baada ya kipindi cha miaka 12 kupita.
Kufuatia kushindwa kufuzu kwa fainali zilizofuata mwaka 2012 Nooij alijiuzulu kazi hiyo Septemba mwaka 201.
 Nafasi yake ilichukuliwa na Mjerumani Gert Engels.
Mnamo April 19 April 2012, alichukuliwa na Santos ya Afrika kusini inayoshiriki ligi kuu ya nchini Afrika Kusini, lakini alifukuzwa kazi desemba 18 2012.
 November 2013, Nooij akaajiriwa na Saint George ya Ethiopia na miezi mitano iliyofuatia yaani April 25 akakubali kazi ya ya kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment