KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 26, 2014

Deni la Munich kwa Dortmund lavuruga uhusiano baina yao (Source DW)

 Waswahili wanamsemo wao usemao ukitaka ubaya dai chako, jambo ambalo limeharibu mahusiano baina ya mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich na Borussia Dortmund, ambao watakutana mwezi ujao katika fainali ya kombe la Shirikisho la soka la Ujerumani – DFB.
Kwa nini? Siyo usajili wa wachezaji tu, hapana ni kwa sababu ya mzozo wa deni linalotokana na mkopo uliodumu mwongo mmoja.
Timu hizo mbili zimekuwa zikishambuliana kwa maneno kuhusiana na mkopo wa kiasi cha euro milioni mbili ambao Bayern iliwapa Dortmund wakati walipokuwa wamekabiliwa na matatizo ya kifedha mwaka wa 2004.
Rais wa Bayern Karl Hopfner anadai Afisa Mkuu Mtendaji wa Dortmund Hans-Joachim Watzke hakusema ukweli alipodai kuwa Bayern wanadai kupewa kiasi kikubwa cha riba kutokana na mkopo huo.
Katika misimu minne iliyopita, Dortmund wameibuka kuwa wapinzani wakuu wa Bayern katika ligi ya nyumbani na Ulaya, huku wakishinda mataji mawili katika mwaka wa 2012 na ligi 2011 kabla ya kushindwa na mahasimu hao wa Munich katika fainali ya Champions League msimu uliopita.
Hata hivyo wamewapiga Bayern magoli matatu kwa sifuri katika Bundesliga hivi majuzi ili kujirejeshea hadhi yao. Afisa Mkuu Mtendaji wa Bayern Karl Heinz Rummenige anasema Bayern haihitaji mkutano wa kilele wa amani na wala haihitaji mkutano wowote na Dortmund.
Bayern ambao wanalenga kurudia mafanikio ya msimu uliopita kwa kushinda mataji matatu, Bundesliga, Champions League na kombe la DFB, wanapambana na Real Madrid Jumanne ijayo katika pambano la marudiano la nusu fainali.

No comments:

Post a Comment