KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, April 25, 2014

Imefahamika: Frank Lampard atasalia darajani msimu ujao

Inaaminika kuwa Frank Lampard yuko katika kuelekea kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu yake ya Chelsea.

Mkongwe huyo wa 'The Blues' atakuwa nje ya mkataba wakati wa kiangazi kama ilivyo kwa wakongwe wenzake mlinzi wa kati John Terry na mlinzi wa pembeni Ashley Cole.

Lakini inavyoonekana ni kwamba Lampard atakuwa wa kwanza kuingia saini katika makabrasha ya mkataba kwa kipindi cha mwaka mmoja wa kuendelea kusalia Stamford Bridge, na inaarifiwa kuwa alikuwa katika mazungumzo na wakuu wa darajani wiki chache zilizopita.

Taarifa zinaarifu kuwa nyota huyo wa kimataifa wa England angeelekea ligi ya Marekani ya MLS msimu ujao, lakini bosi wa Chelsea  Jose Mourinho amekuwa akionekana kutaka kumbakisha kiungo huyo mzoefu katika kikosi chake wakati huu ambapo anapigana kuimarisha kikosi.

No comments:

Post a Comment