KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, May 2, 2014

Hatimaye Chelsea yamsajili Diego Costa kwa pauni milioni 32, na mshahara wa pauni 200,000/



Waswahili wana msemo usemao 'Mgaa Gaa na Upwa hali wali mkavu' ndivyo ilijidhihirisha hii leo kuwa kweli mambo yanawezeka sharti kubwa uweke nia.

Chelsea iliyokuwa ikimuawani kwa muda mrefu kwa miezi kadhaa hatimaye wamempata mchezaji walikuwa wakimfukuzia baada ya hatimaye kukubali kumsajili Diego Costa kutoka katika klabu ya Atletico Madrid.

Costa, ambaye alifunga katika mchezo dhidi ya Blues japo goli la mkwaju wa penati katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliopigwa darajani katikati ya wiki hii, ni mchezaji mlengwa namba moja na anaonekana kutua darajani mapema.

Kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania, zinasema kuwa Chelsea wamefanikisha uhamisho huo baada ya kukubali kufikia dau la uhamisho lilitangazwa na klabu yake la kiasi cha pauni milioni £32.
Costa pia amekubali kimsingi yaliyomo katika maslahi yake binafsi kwa minajili ya kuishi darajani kwa miaka mitano huku akitarajiwa kutangazwa rasimi mwishoni mwa msimu.

Mshambuliaji huyo mwenue umri wa miaka 25 hapo jana aliripotiwa akisema kuwa yuko makini kutoka na kupokea ofa nyingi kabla ya kuamua.

Costa atakuwa akipata kiasi cha pauni milioni £200,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment