Helena Costa raia wa Ureno atakuwa mwanamke wa kwanza
kuwa kocha wa timu ya kulipwa ya wanaume nchini Ufaransa baada ya
kutangazwa na timu ya Clermont Foot 63 kuwa kocha wake mkuu, Jumatano.
Helena Costa mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa ni
meneja wa timu ya taifa ya Iran ya wanawake, akiwa amewahi pia kusaidia
usajili kwa timu ya Celtic na kuwa meneja wa timu ya wanawake ya Qatar.
"Uteuzi wake utasaidia timu ya Clermont Foot 63 kuingia katika kipindi kipya", amesema Clermont.
Clermont inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligue 2 nchini Ufaransa ikibakia michezo miwili kukamilisha msimu wa ligi hiyo.
Clermont itawategemea wachezaji 17 ambao kwa sasa bado wana mikataba na itawaongeza wachezaji chipukizi kutoka timu hiyo.
Olivier Chavanon, amekuwa na uzoefu mkubwa na uelewa wake wa kina wa timu hiyo utasaidia kuwa karibu zaidi mchezoni.
Utambulisho wa meneja mpya wa timu ya Clermont utafanyika Clermont-Ferrand mwisho mwa msimu wa 2013/2014.
No comments:
Post a Comment