Majukwaa ya uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba |
Mtaalamu
wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian
McClemen leo wameanza kukagua ukaguzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Kaitaba mjini Bukoba kablan ya hapo kesho kukagua Uwanja wa Nyamagana tayari kwa maandalizi ya kazi ya uwekaji wa nyasi za bandia.
Viwanja
hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa shirikisho la soka duniani FIFA chini ya mpango wa misaada wa
Goal Projects.
Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili
shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Uwanja wa Kaitaba ni miongoni mwa viwanja ambavyo vilivyofungiwa na TFF baada ya nusu msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara huku amri ya marekebisho ikitolewa kabla ya kuanza duru ya pili la ligi hiyo.
Uwanja huo ulisimamishwa kutokana na majukwaa
yake kuchakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji.
Kwa upande wa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza wenyewe ulikuwa katika mpango huo wa FIFA wa Goal Project 4 tangu awali ambapo kiasi cha dola 630,000 (zaidi ya Sh bilioni moja) kimepangwa kutumika
katika kuukarabati uwanja huo mkongwe wa soka kwa lengo la kuufanya uwe wa kisasa.
Ukarabati huo utajumuisha uwekwaji wa nyasi bandia pamoja na taa kwa ajili ya matumizi ya uwanja huo nyakati za usiku.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema uwanja huo unatarajiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetoa dola 500,000 kwa ajili ya kazi hiyo, huku Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiridhia kuongeza kiasi kingine cha dola 130,000 kwa ajili ya kuuboresha kwa kuuwekea taa, viti na nyasi bandia.
Kwa
Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni
Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na
Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
![]() |
Hii ndio sura ya uwanja wa Nyamagana kwa sasa |
No comments:
Post a Comment