Msumbiji yaichapa Taifa Stars na kupaisha ndoto za kutinga hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika
 |
Taifa Stars ya Tanzania iliyokuwa uwanja wa Zempeto jijini Maputo imeshindwa kutamba mbele ya wenyeji Msumbiji na kuambulia kichapo cha mabao 2-1, na kuyeyusha matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika. Kabla ya mchezo huo Stars ilikuwa ikihitaji ushindi wa ugenini au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili kuwerza kusonga mbele lakini haiukuwa hivyo na kushuhudia dakika 90 zinakamilika wakiwa nyuma ya mabao 2-1. Msumbiji waliandika bao la uongozi dakika 45 likifungwa na Josimar kabla ya Mbwana Samata kusawazisha kunako dakika ya 77 goli ambalo lilidumu kwa dakika 5 kabla ya msumari wa mwisho kwa wenyeji kushindiliwa na Dominguez kunako dakika ya 83. Matokeo hayo nayairejesha vichwa chini Stars ambayo sasa itakuwa haina la kushindania barani Afrika. | |
No comments:
Post a Comment