Pamoja na kustaafu kucheza soka David Beckham adhihirisha mapenzi yake katika mchezo wa Baseball
|
David akiwa na Brooklyn, Romeo na Cruz akiangalia mchezo wa Baseball wakiishabikia Los Angeles Dodgers Alhamisi iliyopita
Anaweza kweli akawa amejiuzulu kucheza soka la kulipwa mwaka uliopita, lakini michezo kwake ni kama imechukua sehemu kubwa ndani ya moyo na maisha ya David Beckham.
Kiungo huyo wa zamani wa LA Galaxy ametumia sehemu kubwa kuwachukua watoto wake Brooklyn, 15, Romeo, 11, na Cruz, 9 kwenda kuangalia mchezo wa Baseball ambao timu yake ya Los
Angeles Dodgers ilikuwa ikicheza huko Dodger Stadium jijini Los Angelos Alhamisi usiku.
Watoto hao wa kiume wa Beckham wameonekana kufurahia mchezo huo wakiwa na baba yao wakati timu yao ya nyumbani ilipoichapa Atlanta Braves 2-1.
Like father, like son: David akifurahi na mtoto Cruz mwenye umri wa miaka tisa
Beckham alikuwa amevalia kapelo ya Dodgers na alipigwa picha akiwa na watoto wake wakizungumza mchezo huo.
Wakati huohuo mama wa watoto hao wanne Victoria alikuwa amesalia nyumbani akiendelea na malezi ya matoto pacha wa kike wenye umri wa miaka miwili Harper.
Majukumu ya baba: Hapa Brooklyn na huku Cruz wakipiga stori kuhusu game
Beckham
amekuwa akijishughulisha na mambo ya maonyesho ya mavazi( underwear collections for H&M) tangu alipoachana na soka Mei 2013.
Katika kipindi chake cha miaka 20 ya uchezaji soka, mbali ya kuichezea na kuwa nahodha wa timu ya taifa ya England, amechezea vilabu kadhaa kama vile Manchester United, Real Madrid, Milan, Los Angeles Galaxy na Paris Saint-Germain.
|
No comments:
Post a Comment