Atakaa wapi? Radamel Falcao akipiga picha na meneja msaidizi Ryan Giggs baada ya kusaini kwa mkopo katika siku ya mwisho ya usajili wa kiangazi |
Paul Scholes ana wasiwasi wa Van Gaal kuwatumia washambuliaji wawili badala ya watatu baada ya kuwasili kwa Radamel Falcao |
Kiungo wa zamani wa Manchester
United Paul Scholes haoni ni kwa vipi meneja wa klabu hiyo Louis van Gaal atawatumia washambuliaji watatu Wayne Rooney, Robin van Persie na ngizo jipya Radamel Falcao katika timu moja.
Scholes
anaamini kuwa Falcao, aliyejiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Monaco katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili ni mchezaji wa aina ya pekee lakini anasisitiza kuwa klabu yake hiyo ya zamani itafanikiwa tu kuwatumia washambuliaji wawili tu kati ya washambuliaji watatu wenye majina.
Ameandika kupitia ukurasa wake katika gazeti la The Indepandent
'Nilipokuwa nikimuona Falcao akiichezea Porto, Atletico Madrid
na Monaco niliona ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa na mwenye rekodi ya ufungaji tofauti kabisa katika dunia hii.
Nani atakalia benchi? Paul Scholes haamini kama Louis van Gaal ataweza kuwatumia washambuliaji wote watatu kwa wakati mmoja.
'Falcao
anaibua ushindani mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya United. Hakuna namna ya kufanya kwa Van
Gaal ya kuwachezesha wote kwa pamoja Rooney, Van Persie na Falcao. Itakuwa wawili kati ya watatu hao jabo ni ngumu kusema kwasasa.'
Scholes
anaamini usajili wa mapesa na kuvutia wa klabu hiyo kiangazi ambao umewaleta Luke Shaw, Ander Herrera, Marco Rojo, Angel di Maria na Danny Blind ndani ya Old Trafford kwa jumla ya pauni milioni £150 umempa Van Gaal kikosi cha ushindi wa taji msimu huu kama si kumaliza katika nne za juu.
'Credit
ziende kwa makamu mtendaji mkuu wa United Ed Woodward, ambaye amemuachia Van
Gaal kikosi ambacho kinaweza kumaliza katika nafasi nne za juu," Amesema Scholes.
'Sidhani kama ushindi wa taji la ligi ni lazima lakini katika Champions League ni dhumuni kuu. Sasa imebaki kwa Van Gaal kutengeneza kikosi.
Licha ya kufurahishwa na ujio wa wacheza wapya, Scholes amesema amehuzunishwa na kuondoka kwa mtoto aliyekulia Old Trafford (academy graduate) Danny Welbeck kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £16 ambaye ameelekea Arsenal hata kama hawezi kufunga magoli 20 katika msimu.
'Danny hawezi kufikisha magoli 20-25 ndani ya msimu lakini anaweza kuifungia Arsenal magoli 10 mpaka 15.'
Matarajio makubwa: Ujio wa wachezaji kama Angel di Maria kumeifanya United kuwa na matumaini ya kumaliza katika nne bora
Danny Welbeck
No comments:
Post a Comment