Inavyoonekana ni kuwa mashabiki wa soka huwa hawapati nafasi ya angalau kukutana na mashujaa wao wanaowapenda, hii ni tofauti kwa klabu ya Villarreal ambayo yenyewe imetoa nafasi kwa mmoja wa shabiki wake kutimiza ndoto yake ya kuichezea klabu hiyo.
Klabu hiyo kubwa nchini Hispania ilikuwa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Celtic hivi karibuni na kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza dogo mwenye umri wa miaka 13 ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kansa Gohan.
Hapo kabla Gohan aliwafahamisha manesi wanamuhudumia kuwa ana ndoto ya kuichezea Villarreal ndani ya uwanja wa Madrigal huku nayo klabu hiyo ikalipokea hilo kwa furaha.
Villarreal imekubali kulipia gharama zote za matibabu ya daraja la VIP kwa Gohan alipokutana na wachezaji katika chumba cha kubadilishia nguo kabla ya mchezo wa Hisani kuchangia watoto wanao sumbuliwa na kansa ambapo wachezaji walifurahishwa mno kukutana naye na kuwa nyuma yake.
Usiku huo ulikuwa mzuri kwa dogo huyo ambaye alifunga goli kupitia mpira wa adhabu ya moja kwa moja baada ya kuonyesha utundu wa kuchezea mpira.
Akifurahia goli hilo alilofunga na wachezaji wenzake wa Villarreal baadaye Gohan alibadilishwa huku akipokea makofi mengi ya mashabiki wa klabu hiyo ambayo ilishinda bao 5-2.
Gohan alifunga goli la kwanza la Villarreal na kupongezwa na wachezaji wenzake
Wachezaji wa Villarreal wakimbeba Gohan baada ya kufunga goli la kwanza
Tabasamu: Gohan anakutana na mashujaa wake wa Villarreal kabla ya mchezo kuanza
Timu hizo mbili zilikubaliana kuunganisha nguvu katika miaka ya hivi karibuni kwa lengo kutunisha mfuko wa kuhudumia watoto wenye kusumbuliwa na maradhi ya kansa.
Kichocheo kikubwa cha makubaliano hayo kilikuwa ni Mchezaji wa zamani wa Villarreal Ernesto Boixader alipoteza mtoto wake kutokana na maradhi hayo kabla ya mchezo wa UEFA Cup dhidi ya Celtic miaka 10 iliyopita.
No comments:
Post a Comment