Javier Hernandez amedhihirisha kuwa yeye ni zaidi ya mchezaji wa akiba (super-sub) ndani ya kikosi cha Real Madrid kufuatia kufunga katika mchezo wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Cornella ukiwa ni mchezo wa Copa del Rey Jumatano.
Nyota huyo wa kimataifa wa Mexico alipewa nafasi katika kikosi cha kwanza na kudhihirisha uwezo ndani ya Real kama ilivyokuwa kwa Manchester United ikiwa ni mara moja tu ndani ya La Liga msimu huu.
Kocha mkuu Carlo Ancelotti amempa nafasi mshambuliaji huyo ya kuonyesha ubora katika Copa de Rey, na kufunga goli ndani ya viunga vya Estadio Municipal de la Via Ferrea.
Amenukuliwa Hernandez akisema"najituma kupata nafasi na natumia uwezo wangu wote nikiwa na Madrid ," alikuwa akiongea na wanahabari baada ya mchezo.
No comments:
Post a Comment