CHAMPIONS LEAGUE GROUP STAGE TO QUALIFY
Braga aishtusha Sevilla, Bremen yakamua
Braga imefanikiwa katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa baada ya kuichapa Sevilla usiku wa kuamkia jumatano wakati ambapo Werder Bremen wakipata bao la dakika za majeruhi katika muda wa nyongeza na kuiondosha Sampdoria.
mchezo kati ya Sevilla dhidi ya Braga nyota wa mchezo huo Lima wa Braga amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matatu pekee yake yaani “hat-trick” katika mchezo ambao Braga wamepata ushindi wa mabao 4-3 na hivyo kufanikiwa kupenya kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3. Braga ya Ureno ilikuwa tayari na ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza na hivyo mabao ya Matheus dakika ya 31 na mabao mengine matatu ya Lima yamewapa ushindi wa jumla wa mabao 5-3 ukiwa ni ushindi wa jumla.
Katika mchezo Sevilla dhidi ya Braga Luis Fabiano alifanikiwa kuandika bao la kwanza huku wakiwa nyuma kwa mabao mawili kunako dakika ya 60 na Jesus Navas kuandika bao la pili na la kusawazisha katika dakika ya 84. baada ya dakika moja Lima akaandika bao lake la pili kabla ya kuandika bao lake lingine la tatu na Frederic Kanoute wa Sevilla katika dakika ya mwisho akifanikiwa kuiandikia Sevilla bao la tatu hata hivyo haikutosha na hivyo Sevilla kuondoshwa katika Europa League.
Sampdoria wakiwa nyumbani wao ambao katika mchezo wao wa kwanza walichapwa kwa jumla ya mbao 3-1 kule Ujerumani na Bremen walikuwa na kazi ya kubadili matokeo wakiwa katika dimba la nyumbani la Luigi Ferraris wamejikuta licha ya kuongoza kwa jumla ya mabao 3-0 mpaka dakika ya 85 hata hivyo mabao ya Markus Rosenberg kunako dakika ya 90 na linginne la Claudio Pizarro katika dakika za nyongeza yamefanikisha Bremen kufuzu katika mabingwa ulaya.
Giampaolo Pazzini alifanikisha kupata mabao mawili ndani ya dakika 13 za mchezo wakati Antonio Cassano akiandika bao la tatu lakini baoa bao la dakika za majeruhi la Pizarro limemfanya aondoke dimbani akionekana shujaa katika mchezo huo.
Partizan Belgrade wao wamefanikiwa kuwachapa Anderlecht kwa jumla ya mabao 3-2 kwa njia ya mikwaju ya penalt katika mchezo uliopigwa Belgium. Baada ya sare ya mabao 2-2 mchezo ukaingia katika hatua ya matuta na wenyeji kupaisha jumla ya penalt tatu .
Partizan walianza kuongoza kwa mabao 2-0 mabao ya Cleo lakini Anderlecht walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Romelu Lukaku na Guillame Gillett
No comments:
Post a Comment