KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 12, 2010

Bobby zamora nje miezi minne kufuatia kuvunjika mguu Mshambuliaji wa Fulham Robert Lester Zamora “Bobby Zamora” atalazimika kuwa nje ya dimba kwa takribani minne kufuatia kuvunjika mguu katika mchezo wa jumamosi wa ligi kuu ya kandanda dhidi ya Wolverhampton Wanderers.
Zamora mwenye umri wa miaka 29 na ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka minne na klabu yake ya Fulham ijumaa alikutana ka kisago hicho katika kukabiliana na Karl Henry licha ya skipper huyo wa Wolves kufanikiwa kuunasa mpira lakini kwa upande wake Zamora mguu wake wa kulia aliokuwa na ankle ukanasa katika miguu ya Karl na kuvunjika.

Katika msimu ulipita Zamora alitikisa wavu mara nane katika michezo ya ligi kuu ya uingereza na mabao matatu katika michezo ya FA Cup huku mengine matatu katika michezo ya Europa League michuano ambayo Fulham walitota katika mchezo wa fainali dhidi ya Atletico Madrid. Alikuwepo pia katika kikosi cha Uingereza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwezi uliopita dhidi ya Hungary mchezo ulipigwa katika dimba la Wembley.

Akithibitisha juu ya hilo meneja wa Fulham Mark Hughes amesema ni kweli kijana wake itamchukua muda mrefu kabla ya kurejea na upasuaji ndio utakuwa na majibu halisi.

No comments:

Post a Comment