Akikaririwa hapo jana mkali huyo wa kikapu anasema
"tumeamua kuwa wachumba na sote kwa pamoja tuna furaha sana"
Akiendelea zaidi kuzungumzia juu ya hilo hapo jana kabla ya mchezo wao dhidi ya Golden state Vujacic anasema "ni jambo zuri na sasa tunatazama mbele juu ya mambo yetu mengine."
Wakala wa mshindi mara tatu wa Grand Slam Sharapova amethibtisha juu ya taarifa hizo kupitia njia ya barua pepe na kuzipeleka Associated Press.
Vujacic amesema wameamua kufunga uchumba huo baada ya kuwa karibu kwa karibu mwaka mmoja sasa .
Vujacic anasema siku ya ndoa ya bado kutangazwa.
Mlinzi huyo wa kikapu toka Slovenia amerejea kiwanjani alhamisi baada ya kuwa katika majeraha kwa karibu juma zima kufuatia kugongana na mchezaji mwenzake wa Lakers Lamar Odom wakiwa mazoezini na kuumia kiwiko wastani wa Vujacic wa points kwa msimu uliopita ni points 2.8 huku akiwa wastani wa rebounds 1.2 katika michezo 67 na hii ni klabu yake ya sita tangu aanze kucheza kikapu.
Sharapova ameshinda kwa mara ya kwanza taji la Wimbledon mwaka 2004 alikpokuwa na umri wa miaka 17. Akaendelea kushinda taji linguine mwaka 2006 taji la U.S. Open na mwaka 2008 akashinda taji la Australian Open na hata kufikia nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa kucheza tennis kwa akina dada kwa viwango vya WTA rankings.
Baada ya maumivu ya hapa na pale ya kiwiko kama ilivyokuwa kwa mchumba wake mpya Sharapova sasa yupo katika nafasi ya 18.

No comments:
Post a Comment