
Mshambuliaji huyo ameipatia timu yake bao hilo pekee katika dakika ya kwanza ya mchezo na kufanya Esperance kuwaondosha Al Ahal ya Misri kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungana mabao 2-2 kufuatia Al Ahal kupata ushindi wa nyumbani wa mabao 2-1 na wao kupata faida ya bao la ugenini.

Esperence ya Tunisian waliwahi kuwa mabingwa mwaka 1994 na sasa wanataraji kukutana dhidi ya mabingwa watetezi TP Mazembe katika mchezo wa fainali .
Mchezo wa kwanza wa fainali unatarajiwa kupigwa kati ya tarehe 29,30 na 31 mjini Kinshansa na mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Tunia Tunisia kati ya tarehe 12,13 na 14 kuamua bingwa wa mwaka huu
No comments:
Post a Comment