KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 29, 2011

Gerardo Martino apiga chini kazi ya kufundisha Paraguay Gerardo Martino mwenye umri wa miaka 48 ameachana na kazi hiyo kufuatia madai kuwa hana uwezo tena wa kuendelea kuifundisha timu hiyo ya taifa huku ikidaiwa kuwa iwezo wake umeshuka hii ikifuatia kupoteza mchezo wa fainali ya Copa America dhidi ya Uruguay.
Kujiuzulu kwake kunakuja baada ya kuitumikia timu hiyo mwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo aliiongoza timu hiyo ya taifa kwenye fainali ya kombe la dunia za mwaka uliopita 2010 nchini Afrika kusini na kuo9doshwa katika hatua ya robo fainali 2010.
Paraguay ilishindwa haikupata ushindi katika mchezo hata mmoja katika muda wa kawaida katika michezo yake ndani ya dakika tisini lakini ilifanikiwa kufika fainali baada ya kuzifunga Brazil na Venezuela katika hatua ya mikwaju ya penati kabla ya kupoteza katika mchezo wa fainali kwa kichapo cha mabao 3-0 toka kwa vijana wa Oscar Tabarez timu ya taifa ya Uruguay wiki iliyopita.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Martino amekaririwa akisema
"I am no longer the coach of the Paraguayan national team as of today.
"I can no longer contribute to everything we imagined when I took the reins of the national team."
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 amekuwa akihusishwa na kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Argentina baada ya kocha Sergio Batista kuondoka lakini hata hivyo chama cha kandanda cha Argentina kupitia Rais wake Julio Grondona kimesema katika siku za hivi karibuni amependekezwa Alejandro Sabella kuchukua nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment