Clint Dempsey ameshangazwa na Bob Bradley kuondoka kama kocha wa timu ya taifa ya Marekani Kiungo wa timu ya taifa ya marekani Clint Dempsey amesema ameshangazwa na kuondoka kwa meneja wake wa timu ya taifa Bob Bradley lakini pia amemtakia kila la kheri katika maisha yake ya baadaye.
Bob Bradley aliachiliwa kuondoka kama meneja wa timu ya taifa ya marekani alhamisi huku taarifa hizo zikionekana kumshangaza Dempsey asiamini macho yake.
Kiungo Clint Dempsey alikuwa hajui lolote alipoulizwa na mtandao wa Goal.com kuhusu kutoa maoni yake juu ya kuondoka kwa meneja wake huku akisema ameshangazwa na taarifa hizo za kuondoshwa kwa Bob Bradley
Lakini pia amesema amehuzunishwa na kuondoka kwake ."I'm sad to see him go, But I wish him the best in the future. He's a good coach and I know he'll do well."
Dempsey amekuwa miongoni mwa nyota wa timu ya taifa ya marekani chini ya Bradley na alikuwepo katika kikosi cha meneja huyo kilichoshinda kombe la dhahabu mwaka 2007 pamoja na kikosi kilichopata mafanikio kilichofika katika hatua ya fainali ya “Confederations Cup” mwaka 2009, na vilevile akiwa ni mchango mkubwa katika michezo ya fainali ya kombe la dunia mwaka jana 2010 nchini Afrika kusini.

No comments:
Post a Comment