KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 20, 2012

MILOVAN CIRKOVIC: ABDALAH JUMA KUZIBA PENGO LA OKWI, KIGI KESHO KUZIBA PENGO LA MAFTAHA














Kocha mkuu wa Simba Milovan Cirkovic
 Kocha wa Simba Milovan Circovich amewatoa wasiwasi wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo katika changamoto ya kusaka taji la michuano ya Kagame huku akisema wamekuwa wakiendelea na mazoezi vizuri na Simba ipo tayari ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Vita club ya DRC.
Circovich licha ya kwamba mchezo wa kesho kutokuwa na umuhimu wowote kwao kwakuwa timu hiyo imeshaingia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo bado watahitaji ushindi .
Amesema kimsingi timu ipo katika hali nzuri licha ya kukabiliwa na pengo mlinzi wa kushoto Amir Maftaha ambaye amepata matatizo katika kidole cha mkononi lakini kocha huyo amesema pengo lake litazibwa na Kigi Makasi.

 Shomari Kapombe alikuwa na maumivu kidogo lakini Circovich amesema kwasasa anaendelea vizuri na amezungumza naye ameonyesha kuwa yuko fiti na tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho lakini ameshindwa kuthibitisha kama atamtumia ama hapana.

Akizungumzia kikosi cha Vita club ya DRC kocha huyo wa Simba amesema anajua kuwa Vita ni timu nzuri lakini haiogope na waanamini wamejiandaa vizuri na hawaihofii timu yoyote kwenye kagame.
Amesema Simba kwasasa ina pengo la Emmanuel Okwi ambalo limeathiri sana sehemu ya ushambuliaji lakini katika kuhakikisha anafanikiwa kuziba pengo hilo kwasasa anamtengeneza Abdalah Juma ili aweze kuliziba pengo hilo.

Amewataka mashabiki wa Simba kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho kocha anajaribu kutengeneza timu kwasababu wameondokewa na wachezaji muhimu kama Patrick Mafisango aliyefariki dunia May 16 na Emmanuel Okwi aliyekwenda kujaribu kucheza soka barani ulaya.

No comments:

Post a Comment