KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 27, 2012

THOM SAINTFIET AKUNWA NA BARTHEZ.

Mlinda mlango wa zamani wa mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba ambaye kwasasa anadakia kwa wapinzani wao wakubwa katika soka la Tanzania Yanga Ally Mustafa 'Barthez' amemkuna vilivyo kocha wake Thom Saintfiet na ameanza kuumiza kichwa juu ya huduma yake ndani ya timu yake.
Kocha huyo wa mabingwa watetezi wa kombe la Kagame jana alimtumia Bartez kwa mara nyingine tena baada ya kudaka katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mafunzo na kufurahishwa na kiwango chake huku akusema kuwa bado anafikiria juu ya huduma yake katika kikosi cha Yanga.
Mashabiki wengi wa Yanga jana walisikika wakisema kuna haja ya kiwango cha mlinda mlango huyo kulindwa kisiporomoke haraka na njia pekee ya kufanikisha hilo ni apewe nafasi ya  ya kulinda lango la Yanga licha ya kuwa mlinda mlango namba moja wa timu hiyo kuwa ni Yaw Berko.
Akiongea na Rockersports Saintfiet amesema mlinda mlango huyo yuko katika kiwango kizuri isipokuwa alikuwa hapewi nafasi ya kulinda lango katika timu ya Simba kiasi kuonekana si lolote mbele ya Juma Kaseja licha ya kuwepo katika klabu ya Simba kwa kipindi kirefu cha mkataba wake.
Barthez jana alikuwa akilinda lango la Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Kagame dhidi ya APR ya Rwanda akicheza dakika zote za mchezo na kuonekana kuwafurahisha mashabiki wa Yanga baada ya kuokoa magoli matatu ya wazi lakini pia akiwa mtulivu langoni.
Hata hivyo katika mchezo wa kesho Yanga inatarajia kumrejesha langoni Yaw Berko ambaye inaarifiwa maumivu ya mguu wake yameondoka.
Barthez alianza kudakia Yanga katika mchezo dhidi ya Mafunzo mchezo wa robo fainali akiingia kipindi cha pili baada ya Berko kuumia.
Ally mustafa Barthez amesajiliwa na Yanga msimu huu baada ya mktaba wake na Simba kumalizika na Simba kumtupia virago vyake.

No comments:

Post a Comment