KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 8, 2012

TP MAZEMBE YAKAMATWA NYUMBANI NA ESPERENCE MCHEZO WA KWANZA NUSU FAINALI YA MABINGWA


 Esperance ya Tunisia imefanikiwa kupata sare ya bila mabao dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya vilabu bingwa barani Afrika mchezo uliofanyika usiku huu.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kiwango sawa kiasi matokeo ya sare kuonekana kama yalistahili.
Mazembe, licha ya kumliza mchezo wakiwa na upungufu wa mchezaji mmoja baada ya Stopila Sunzu kutolewa kwa kadi nyekundu iliyotokana na kupewa kadi mbili za njano.
Matokeo hayo ya leo ya Lubumbashi sasa yataufanya mchezo wa marudiano kuwa mgumu kule Tunisia siku 14 zijazo.
Mshindi wa mchezo huo atakutana na ama Sunshine Stars ya Nigeria au Al Ahly ya Misri katika mchezo wa fainali.
Sunshine na Ahly zilikwenda sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Nigeria jumamosi na hivyo kutoa nafasi kubwa kwa mashetani wekundu wa Cairo kupenya na kutinga fainali.
TP Mazembe na Esperance zimekuwa zikigawana ubingwa wa vilabu Afrika katika kipindi cha miaka 3 iliyopita huku Mzembe wakichukua mara mbili 2009 na 2010.

No comments:

Post a Comment