KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 7, 2012

NI RONALDO NA MESSI EL CLASSICAL WASHINDANA KUFUNGA MABAO NA KUPELEKEA SARE YA 2-2 NOU CAMP.


Lionel Messi na Cristiano Ronaldo usiku huu walikuwa wakibadilisha kuonyesha ushujaa wao wa kupachika mabao katika mchezo uliochezwa katika dimba la Nou Camp huku kila mmoja akifunga mabao 2 mchezo uliozikutanisha Barcelona na Real Madrid ukiwa ni mchezo mkubwa katika soka la Hispania maarufu kama  Clasico.
Kikosi cha Tito Vilanova cha Barca kilikuwa kikiingia katika mchezo huo kikiwa kinaongoza ligi hiyo kwa utofauti wa 8 dhidi ya wapinzani wao wakubwa katika soka la nchi hiyo na hivyo kuendelea na rikodi yao nzuri ya asilimia 100 baada ya michezo 6.
Alikuwa ni Cristiano Ronaldo aliyeanza kufungua mlango wa magoli akiweka rekodi iliyotukuka ya kufunga katika kila mchezo unaozikutanisha timu hizo na mara hii ikiwa ni mchezo wa sita mfululizo wa Clasico ambapo amekuwa akizifumania nyavu.
Hata hivyo Lionel Messi alifanikiwa kusawazisha kwa mpira uliorudi kwa bahati mbaya katika harakati za kuokoa na baadaye akafanikiwa kuandika bao la pili kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kuwapa uongozi Barcelona wa mabao 2 kunako dakika ya 60 ya mchezo kabla ya Ronaldo kusawazisha katikati ya kipindi cha pili na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Kiungo wa Barca Andres Iniesta alipewa nafasi ya kuanza katika mchezo huo hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu alivyofanya hivyo kwa mara ya mwisho katika mchezo wa Supercopa dhidi ya Real mwezi August, ilhali Adriano akisaidiana na Javier Mascherano katika sehemu ya kati ya ulinzi kuziba mapengo ya Gerard Pique mwenye maumivu ya mguu na Carles Puyol anayesumbuliwa na maumivu ya mkono.
Kocha wa Madrid Jose Mourinho alikifanyia mabadiliko kikosi chake tofauti na kile kilicho ibuka na ushindi wa mabao 4-1 nyumabani kwa Ajax katika mchezo wa michuano ya ligi ya mabingwa mchezo uliofanyika jumatano, ambapo Sami Khedira, Mesut Ozil na Angel Di Maria walichukua nafasi za Michael Essien, Kaka na Jose Callejon.
Kwa  matokeo hayo  Barcelona inaendelea kusalia katika usukuani wa ligi hiyo wakiwa na zaidi ya points 8 kama ilivyokuwa kabla ya mchezo ikiwa ni baada ya michezo 7.

No comments:

Post a Comment