KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 1, 2014

Frank Lampard na Ashley Cole wakutana Etihad kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka kwa pamoja Stamford Bridge msimu uliopita

Wakali wa zamani wa Chelsea Frank Lampard na Ashley Cole waliungana tena baada ya mchezo uliotoa matokeo ya sare baina ya Man City na Roma
Frank Lampard na Ashley Cole waliungana tena katika mchezo uliozikutanisha Manchester City na Roma usiku wa jana Jumanne.

Nyota hao wa zamani wa Chelsea ambao waliondoka Stamford Bridge kiangazi iliyopita walikutana Etihad Stadium ambapo walipiga picha ya kumbukumbu.

Akitupia picha hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter hii leo asubuhi Cole aliambatanisha pia ujumbe uliosomeka 

'Ilikuwa furaha sana kukutana na Lamps usiku wa jana!! namtakia kila la kheri katika kila la kheri City na New York. Such a goalmachine!!'

Lampard and Cole embraced shortly after the full time whistle at the Etihad Stadium on Tuesday night
Lampard na Cole walikumbatiana muda mfupi baada ya mchezo kumalizika katika uwanja wa Etihad usiku wa jana
Cole will have been the happier of the two Chelsea legends as Roma came away from England with a point
Cole alikuwa mwenye furaha baada ya kukutana na nyota mwenyezake wa zamani walipokuwa  Chelsea Lampard

Muda mfupi baada ya kukutana Cole aliandika kupitia ukurasa wake wa tweeter 'Hisia za ajabu kucheza tena nchini England dhidi ya Lamps!! siku zote ni vigumu kucheza dhidi ya ya City lakini ni bora kupata alama moja.' 
Lampard kwasasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Manchester City ambapo alijiunga na New York City FC ilhali Cole alisaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Roma mwezi July baada ya wote wawili kuruhusiwa kuondoka Chelsea mwishoni kwa msimu uliopita.
Mlinzi huyo wa zamani wa kushoto wa Chelsea amekuwa ni mchezaji wa 11 kutokea katika nchi ya England kucheza ligi ya mabingwa Ulaya baada ya jana akicheza kwa mara ya kwanza katika dimba la Etihad.
The former Stamford Bridge duo helped Chelsea win the Premier League, Champions League and FA Cup
Wakati huo wakiichezea Chelsea yenye maskani yake Stamford Bridge wawili hao waliisadia Chelsea kushinda mataji la Premier League, Champions League na FA