KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, September 30, 2014

Mignolet hana wasiwasi na Valdes

Simon Mignolet sina wasiwasi na Valdes
Golikipa wa Liverpool, Simon Mignolet, amesema hasumbuliwi na taarifa klabu hicho cha ligi ya Uingereza kitasaini mlinda lango shupavu Victor Valdes, ambaye kwa sasa hana makao baada ya kuondoka Barcelona musimu uliopita.
Mignolet amejipata chanzo cha lawama baada ya kufungwa kwenye mechi tano kati ya sita ambazo Liverpool wameshiriki kwenye ligi ya Premier muhula.
Victor Valdes
Uvumi umehusisha Liverpool na sahihi yake Valdes ambaye ni ajenti huru ikiwa ataweza kudhihirisha usawa wake baada ya jeraha mbaya la goti ambalo lilikatiza muda wake Barcelona mapema musimu jana.
Mignolet ametaja ripoti hizo kama tuhuma huku akitangaza hana wasiwasi yeyote kuhusu nafasi yake.
“Ukiangalia wachezaji wote waliohusishwa na Liverpool, basi kungelikuwa na kikosi kingine uwanjani. Unapochezea timu kubwa, ni lazima utarajie taarifa kama hizi na langu ni kufanya kadri ya uwezo waku wiki baada ya wiki,” Mignolet aliongeza.