KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 1, 2014

Nani kati ya Messi na Cristiano Ronaldo anaelekea kuvunja rekodi ya Raul ya kufunga magoli mengi Ulaya, huku Ronaldo akiwa na nafasi nyingine usiku huu

Cristiano Ronaldo anaelekea kuvunja rekodi ya Raul ya kufunga magoli mengi Ulaya
Cristiano Ronaldo anaelekea kusaka rekodi ya ufungaji bora wa kipindi chote katika michuano ya vilabu ULaya mjini Bulgaria katika dimba la Vasil Levski huku kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti akisema kuwa 
'Ni mchezaji bora kuliko wachezaji wote aliowahi kuwafundisha.'
Maneno hayo ya kumbeba mshambuliaji huyo yakiwa pia ni pongezi kwake yanakuja ikiwa no Ronaldo amesalia na magoli matatu tu kuifikia rekodi iliyowekwa na Raul katika Champions League ambayo ni ya magoli 71.
Mshambuliaji huyo ambaye mashambiki wa Manchester United wameanza kujaribu kuwasha moto wa kitaka arejee Old Trafford wakitumia kitambaa kilichorushwa na ndege angani chenye urefu wa futi 20 mwishoni mwa wiki mpaka sasa ana jumla ya magoli 68 katika Champions League huku akiwa na nafasi ya kuifikia na kuipita rekodi hiyo ya nahodha huyo wa zamani wa Real Madrid.
Ingawa magoli yaliyosalia kuvunja rekodi hiyo yakionekana ni mengi katika mchezo mmoja lakini kwakuwa amekuwa na rekodi nzuri ya kupiga magoli matatu katika mchezo mmoja yaani hat-tricks mara 25, Ronaldo anaweza kufikia rekodi hiyo usiku wa leo.
Messi pia anafukuzia kuivunja rekodi hiyo baada ya usiku wa jana kufunga goli katika mchezo dhidi ya Paris Saint-Germain.
Ronaldo alimshinda Messi msimu uliopita kwa kufunga magoli 17 katika jumla ya michezo 11.

ALL-TIME TOP EUROPEAN CUP GOALSCORING RECORD 
1. Raul - 71 goals
2. Cristiano Ronaldo - 68
2= Lionel Messi - 68
4. Ruud van Nistelrooy - 56
5. Thierry Henry - 50
6. Alfredo Di Stefano - 49
7. Andriy Shevchenko - 48
8. Eusebio - 46
8= Filippo Inzaghi - 46 
10. Didier Drogba - 42 

No comments:

Post a Comment