Sturridge anataka
kucheza kama mshambuliaji wa kati Chelsea 2012-13
mshambuliaji wa Chelsea Daniel
Sturridge ameweka wazi juu ya nia yake ya kucheza sehemu ya ushambuaji wa kati
katika klabu yake msimu ujao kufuatia kuondoka kwa Didier Drogba.
mshambuliaji huyo kwasasa yuko katika
timu ya GB katika michuano ya Olympics, na alikuwa akitumika sehemu ya kiungo
wa pembeni katika msimu wa 2011-12 mna kufunga jumla ya mabao 13 katika
michuano yote
amenukuli wa akiongea na talkSPORT
akisema
"nimekuwa nikisubiri fursa hiyo
ya kushambulia toka kati tangu najiunga na Chelsea na nina matumaini msimu
nityakuwa ni miongoni mwa wachezaji wa kati ambapo nitaonyesha uwezo wangu nina
imani meneja atanipa nafasi. "
mchezaji huyo wa zamani wa City
player kwasasa anakabiliwa na ushindan I mkubwa katika sehemu ya ushambuliaji
kufuati katika majira haya ya usajili klabu hiyo kumuongeza Marko Marin, Eden
Hazard na kaka yake Thorgan, lakini anasema anafurahia mabingwa hao wa soka
ulaya kuongezxa nguvu kikosini.
Giroud:Nashawishika Arsenal
itakuwa moto
mshambuliaji wa washika mitutu wa Arsenal
Olivier Giroud anamatumaini kuwa timu yake mpya itawashangaza watu msimu
itakapo twaa taji.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 25 hakuwashanga watu kuongezwa katika kikosi hicho baada ya kuisaidia Montpellier
katika ligi ya soka nchini Ufaransa ya msimu uliopita.
Giroud alimaliza msimu aliungana na
mshambuliaji wa PSG Nene kuwa wafungaji
bora wakifunga jumla ya mabao 21 kila mmoja lakini pia akipiga pasi za mwisho
zilizo zaa magoli tisa lakini pia akitoa msaada katika timu yake ya taifa ya
Ufaransa katika michuano ya Euro 2012.
amenukuliwa akisema aliona mambo
mengi yenye kufanana kati ya Arsenal na Montpellier jambo ambalo limekuwa ni
sababu kubwa ya kukubali kujiunga na klabu hiyo toka pande za kasakazini mwa
jiji la London.
Chelsea yathibitisha
kumtoa De Bruyne
Chelsea imethibitisha kuwa Kevin De
Bruyne amejiunga na Werder Bremen kwa mkopo wa muda mrefu.
De Bruyne mwenye umri wa miaka 21
alijiunga na Chelsea mwezi January kwa ada ya pauni ya milioni £6.7 lakini
alikopeshwa kwa Genk mpaka kumalizika kwa msimu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Belgium alikuwa
katika mazoezi na Blues majira haya ya kiangazi lakini klabu hiyo imeamua
kumkopesha tena kwa lengo la kumuongezea uzoefu zaidi.
taarifa katika mtandao wa klabu hiyo
imesema
"winga huyu sasa ataendelea
kujenga uwezo katika Bundesliga sehemu
ambayo anategemea kupata nafasi ya kuchukua nafasi ya Marko Marin."
De Bruyne anatazamiwa kupata
mafanikio katika klabu ya Werder Bremen.
Busquets azungumzia juu
ya ubora wa Song
kiungo wa Barcelona Sergio Busquets amesema
angependelea kuona kiungo wa Arsenal Alex Song akijunga na Catalan.
Kuondoka kwa Seydou Keita kuelekea
katika klabu moja huko uchina ya Dalian Aerbin mapema majira haya ya kiangazi
kumeacha pengo katika sehemu ya kiungo na Busquets anaamini Song ambaye mkataba wake na Arsenal unatarajiwa
kumalizika mwaka 2014 atakuwa amepeleka ushindani mkubwa katika kikosi chao.
amenukuliwa akisema
"Song ni mchezaji mzuri sana
anajituma na ananguvu" "yuko kijana toka Barca B Sergi Roberto anaandaliwa
lakini nadhani ni vizuri kuwa na chaguo lingine toka ndani.
Busquets amerejea katika mazoezi wiki
hii baada ya kutoa msaada katika timu taifa ya Hispania katiika Euro 2012.
Kikosi cha Barca kitaungana tena hapo
kesho huku Jordi Alba, Cristian Tello na Martin Montoya wakirejea toka katika
michuano ya Olympic mapema kuliko ilivyo tarajiwa.
Barcelona inaendelea na michezo yao
ya maandalizi ya msimu na jumamosi watakuwa na mchezo dhidi ya timu iliyofanya
usajili wa mapesa mengi msimu huu Paris St-Germain.
Wachezaji watimuliwa
mashindanoni
Timu ya mpira wa miguu ya Uswizi
imemfukuza beki wake Michel Morganella kutoka mashindanoni kwa kutuma ujumbe wa
ki-ubaguzi wa rangi akitumia mtandao wa Twitter.
Mchezaji huyo alituma ujumbe
ukiwalenga watu wa Korea ya kusini kwa ujumla kupitia Twitter baada ya Timu
yake kupoteza mechi dhidi ya Korea ya kusini 2-1 jumapili iliyopita.
Tangu hapo mtandao huo umefutwa na
beki huyo kuomba radhi, akisema kweli, nilikosea sana baada ya matokeo
yasiyoridhisha, alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 23.
Morganella aliongezea kusema kua:
"ningependa kuwaomba radhi raia wote wa Korea ya kusini na timu yao,
vilevile ujumbe wa Uswizi na mchezo wa mpira kwa ujumla nchini Uswizi."
Mapema mwezi huu, mwanariadha wa
Ugiriki wa kuruka hatua tatu kuelekea mchangani Paraskevi Papachristou
alitimuliwa kutoka kwenye kikosi cha Olimpiki cha nchi yake kufuatia matamshi
aliyoyatoa kupitia Twitter yaliyoonekana kuwa ya kiubaguzi wa rangi.
Kocha mkuu wa Kikosi cha Uswizi Gian
Gilli alisema kua Morganella, anayecheza soka yake ya kulipwa na klabu ya
Italia -Palermo ameidhalilisha timu nzima. Kocha huyo amesema kua alibagua,
katukana na kukiuka hadhi ya raia na wachezaji wa timu nzima ya Korea ya
kusini.
Inter yapata wamiliki
wa bara Asia
Klabu ya Uitaliano Inter Milan
inasema kua kundi la wawekezaji kutoka Uchina limejitokeza kua wawekezaji wa
pili kwa ukubwa wa kumiliki hisa za klabu hiyo.
Katika taarifa ya Internazionale
Holding,kampuni mama inayosimamia masuala yote yanayohusiana na klabu imesema
kua kundi hilo limetangaza kua litamiliki sehemu ya hisa lakini kwamba familia
ya Moratti itaendelea kumiliki sehmu kubwa ya biashara.
Taarifa hio imesema kua uwanja mpya
utajengwa chini ya ushirikiano na sehemu ya China Railway Construction
ikitazamiwa kukamilishwa mnamo mwaka 2017.
Klabu hio imetangaza kua Kamchi Li,
Kenneth Huang na Fabrizio Rindi wote watakua wakurugenzi kwenye bodi kutokana
na uwekezaji huu.
Inter ndio klabu ya hivi karubini
kuvutia wawekezaji kutoka barani Asia. Klabu ya jijini London na Ligi kuu ya
Premiership Queen's Park Rangers ina milikiwa na Tony Fernandes, huyu akiwa
mmiliki wa kampuni uya ndege baranoi Asia, Air Asia, baada ya kukamilisha
ununuzi wake mwaka jana.
Arsenal kusajili wawili
kwa mpigo
Arsenal inajitahidi kukamilisha
utiaji saini wa makubaliano ya mkataba wa kudumu na mchezaji Santi Cazorla
kutoka klabu ya Malaga pamoja na mcheza kiungo mwenzake Nuri Sahin anayeingia
kwa makubalino ya mkopo kutoka klabu ya Real Madrid.
Mpango wa kuhama kwa mchezaji wa Timu
ya Taifa ya Uhispania Cazorla mwenye umri wa miaka 27 kumekua na utata wa shida
ya fedha inayoikumba klabu ya Malaga hata hivyo anatazamiwa kupitia utaratibu
wa afya wiki hii.
Mcheza kiungo wa timu ya Taifa ya
Uturuki mwenye umri wa miaka 23 Nuri Sahin atajiunga na Arsenal chini ya mpango
wa mkopo wa mwaka mmoja na Real Madrid.
Lililobaki ni baina ya mchezaji Sahin
kukubaliana na klabu ya Arsenal juu ya malipo na marupurupu. Kuna uwezekano
mkubwa kwa wachezaji hawa kuhitimisha utaratibu huu kabla ya msimu mpya kuanza.
Bado Sahin hajapangiwa siku ya
kufanyiwa majaribio ya afya. Arsenal inaanza msimu mpya kwa pambano la ugenini
dhidi ya Sunderland mnamo tareh 18 Agosti.
Tayari Gunners imewasajili wachezaji
wawili mshambuliaji Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne na mshambuliaji wa
Ufaransa Olivier Giroud aliyekuwa akichezea klabu ya Montpellier.
Pamoja na hayo yote wingu zito bado
limegubika majaliwa ya nahodha Robin van Persie, ambaye ametamka kua
hatoongezea mkataba wake unaomazika mwaka 2013.
Usajili wa wacheza kiungo Cazorla
pamoja na Sahin ingawa hakuna uhusiano na mizengwe ya Van Persie lakini
umechagizwa na habari kwamba mcheza kiungo wa Arsenal Jack Wilshere hatoweza
kucheza kabla ya mwezi oktoba kutokana na jeraha la goti.
Cazorla aliyejiunga na Malaga kutoka
klabu ya Villarreal mwaka mmoja tu uliopita ana urefu wa futi 5 inchi 6 na
ameichezea timu ya Taifa ya Uhispania mwaka 2008 na kwenye mashindano ya Ulaya
ya mwaka 2012.
Sahin alisajiliwa na Real Madrid kutoka
Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka sita mnamo mwezi May 2011 lakini
ameshindwa kupata nafasi katika kikosi Mourinho ambapo kocha huyo ameweza
kumruhusu aondoke tu ila kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment