Kocha msaidizi
wa timu ya vijana ya wachezaji wenye
umri chini ya miaka 17 Serengeti Boyz Jamhuri Kihwelu Julio amekipongeza chama
cha soka cha mkoa wa Mbeya MRFA kwa kuandaa kambi ya timu hiyo ya vijana mkoani
humo na kuwaandalia michezo kadhaa ya kujipima nguvu.
Akiongea na
Rockersports akiwa mkoani humo Julio amesema kambi hiyo imewasaidi sana
kiufundi kwani wachezaji wake mbali ya mazoezi mazuri wanayopata pia wamekuwa
katika muda mzuri wa kupumzika.
Serengeti
Boys inatarajia kucheza dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Misri mchezo ambao
umepangwa kucheza Oktoba 14 mwaka huu ambao utapigwa nchini Tanzania kabla ya
mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
Mshindi baada ya mechi hizo mbili ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo ya
mwisho kabla ya kwenda Morocco.
Julio amesema
kambi yao ya mkoni Mbeya imekuwa nzuri kwani wamekuwa wakicheza na timu nzuri
na ambazo zimekuwa zikiwapa mazoezi ya nguzu na kurekebisha makosa katika
michezo mingine pia wachezaji wamekuwa wanakula chakula kingi jambo ambalo ni zuri kujenga afya na nguvu ya mchezaji.
Amevitaka vyama
vingine vya soka vya mikoa kuiga mfano wa viongozi wa soka wa mkoa wa Mbeya ambao
wamekuwa wakiwapa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapangia michezo
mizuri huku pongezi kubwa akizipeleka kwa mwenyekiti wa MRFA Selemani Ayubu pamoja
na viongozi wengine wa MRFA.
Kikosi hicho
cha Serengeti kimecheza michezo miwili ikiwa ni pamoja na Tanzania Prisons
pamoja na Mbozi United lakini pia wanatarajia jumatatu kucheza dhidi ya Mbeya
City kabla ya kuelekea Tukuyu mkoani humo kucheza mchezo mwingine Alhamisi kwa
mchezo mwingine kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.
Katika hatua nyingine timu hiyo imefungwa bao 1-0 na Mbozi United katika mfululizo wa michezo yao ya kujipima nguvu mchezo uliopigwa jumapili hii.
BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment