Giggs: Usajili wa Van Persie,Manchester
United imesajili mchezaji wa kiwango cha dunia
Ryan Giggs ana
matumaini kuwa usajili wa Robin Van Perise , Manchester United imesajili "world-class
star" na kwamba Robin van Persie ataisaidia sana United kuelekea katika
taji la 20 msimu huu.
Wakati United ikipoteza taji kwa majirani zao Manchester
City kwa utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa msimu uliopita, mwingereza huyo mwenye asili
ya Wells anaamini Van Persie amekwenda kuepeleka mazuri baada ya kuifungia
Asernal jumla ya mabao 30 katika msimu uliopita.
Mshambuliaji
huyo aliyeigharimu United jumla ya pauni za kingereza milioni 22 anaonekana kuwa ni katika mpango wa meneja Sir
Alex Ferguson wa kusajili vijana wenye
kiwango.
Tayari Van
Persie ameshaifungia united jumla ya mabao manne jambo ambalo limemfanya Giggs kuamini kuwa United imelamba dume.
Amenukuliwa na
Sky Sports News akisema
"mabao
ambayo Van Persie alichoonyesha kwa ujumla ni wazi kuwa ni mchezaji wa mchezaji
wa kiwango cha dunia.
"sera
ya meneja kwa kipindi cha miaka 10 mpaka 15 ni kusajili vijana wachanga na
kuwaendeleza yokuwa kwa Cristiano [Ronaldo], na Wayne [Rooney].
"lakini
Robin tayari amesha dhihirisha kuwa tayari katika
kiwango cha dunia . ameonyesha hilo katika michezo michache na nataraji mengi
yanakuja."
Mshambuliaji
wa zamani wa Chelsea Didier Drogba amesema kuwa ataendelea kusalia nchini china
na akiwa huko amedhamiria kuisaidia nchi yake ya Ivory Coast kushinda taji la Africa
Cup mwakani na kucheza soka la kiushindani.
Mshambuliaji
huyo wa sasa wa Shanghai Shenhua ndiye aliyefunga goli la penati katika mchezo
wa ushindi wa mabao 4-2 jana mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya
Afrika dhidi ya Senegal mjini Abidjan.
Amesema kuwa
kwasasa anaweka mawazo yake katika hilo na kuwataka mashabiki wa soka kukaa mkao
wa kula na kusisitiza kuwa si tu yuko
barani Asia kucheza soka la ngazi ya klabu l,itakalo mpeleka kustaafu , bali
pia kutoa msaada kwa taifa lake.
Amenukuliwa na
gazeti la L‘Equipe akisema
"kwa
kuelekea katika fainali za mataifa ya Afrika 2013 , nitafanya kila kitu
kuendelea kuwa na kiwango cha kiushindani nikiwa nchini china. Msiwe na
wasiwasi,"
Wakati matokeo
ya mchezo yakisomeka 2-2, Drogba droba alifanikiwa kuandika bao la tatu kabla
ya Max Gradel kuongeza kika tano mpira kumalizika.
Kiungo wa Everton
Marouane Fellaini ametanabaisha kuwa yuko katika mtazamol wa kuondoka katika
klabu yake msimu ujao wa majira ya kiangazi.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga Goodison Park akitokea Standard Liege ya
Ubelgiji September 2008, tayari ameshafun ga jumla ya mabao mawili katika
kikosik cha meneja David Moyes msimu huu.
Fellaini alisaini
kuichezea klabu yake ya Everton mkataba wa miaka mitano November 2011 lakini
mchezaji hnuyo wa kimataifa wa Ubelgiji amesisitiza kuwa huu utakuwa ni msimu
wake wa mwisho ndani ya klabu hiyo.
Amenukuliwa akisema
"sasa
naanza msimu wangu wa tano na Everton, huu utakuwa msimu wangu wa mwisho
kimeona kila kitu mwezi januari au mwisho wa msimu nitakuwa naangalia klabu
nyingine."
No comments:
Post a Comment