Iniesta kukosa michezo mitatu
Nyota wawili
wa kimataifa wa Hispania Andres Iniesta na Jordi Alba wamerejea katika vilabu vya kutoka katika
majukumu ya kimataifa wakiwa na majeraha na ugonjwa licha licha ya kumaliza dakika 90 katika mchezo wao wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Georgia jumanne iliyopita.
Imeelezwa kuwa
Iniesta alipatwa na matatizo ya msuli katika mguu wake wa kulia na taarifa za
madaktari wa klabu yao ya Barcelona zimethibitisha kuwa atakuwa
nje ya uwanja ndani ya kipindi cha kuanzia siku 10 mpaka 15.
Kiungo huyo anatazamiwa kurejea
dimbani katika michezo wa ligi ya Hispania maarifu kama ‘La Liga’ dhidi ya Getafe
na mchezo mwingine dhidi ya Granada katika uwanja wa nyumbani Camp Nou lakini
pia katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Spartak Moscow Jumatano ijayo.
Kwa upande
wa Jordi Alba kuna wasiwasi wa kutokuonekana dimbani katika mchezo dhidi ya Getafe
lakini huenda akawepo katika jiji la Madrid kama hatawekwa benchi.
Wakati hayo
yakiwa hivyo Carlos Puyol amebandika picha yake katika ukurasa wa ‘Twitter
sporting’ akionekana kuvaa kitu kama kinyago kuzuia jeraha lake la taya ambalo
limekuwa likimsumbua na amekuwa akiendelea kufanyiwa matibabu.
Pazzini
ataka AC Milan kukomaa na ushindi mnene
Mshambuliaji mpya wa AC Milan Giampaolo Pazzini ametaka wachezaji wenzake kuendelea kukaza uzi
uleule walioanza nao katika mchezo wa pili wa ligi kwenda nao msimu mzima kama kweli wanataka kupata mafanikio
msimu huu.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ katika
mchezo dhidi ya Bologna ukiwa ni mchezo wake wa pili tangu ajiunge na Milan na
anataka kikosi chake kujiweka katika nafasi nzuri katika kipindi hiki cha
mapumziko ambacho nchi mbalimbali ziko katika michezo ya kimataifa.
Amenukuliwa na
'Milan channel' akisema
“Milan lazima
kila mara iwe imeweka dhamira ya ushindi na tunatakiwa kuwa na uwezo wa kufunga
mabao mengi".
"jumamosi
tunakabiliana na Atalanta tunapaswa kimchezo kuwa katika asilimia 100".
Milan kwasasa
iko katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Italia ‘Serie
A’ kufuatika kushinda mchezo mmoja na kufungwa mmoja baada ya
michezo miwili waliyokwisha kucheza tangu kuanza kwa ligi ya soka ya Italia.
Bentley: Bado naweza kuichezea England
Winga wa Tottenham
David Bentley amedai kuwa bado ana kiwango kizuri cha kuitumikia timu ya taifa
ya Uingereza maarufu kama Simba watatu, kauli ambayo imekuja kufuatia kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya ligi kuu ya Urusi ya FC Rostov.
Winga huyo
mwenye umri wa miaka 28-ameelekea huko baada ya taarifa kusema kuwa ameshindwa
kulinda kiwango chake White Hart Lane baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa ada
ya uhamisho ya pauni milioni €19 akitokea Blackburn Rovers mwaka 2008.
Winga huyo
ameichezea Spurs michezo 48 ambapo katika michezo yote hiyo amefanikiwa kuzifumania nyavu mara tatu tu
kabla ya kupelekwa kwa mkopo katika vilabu vya Birmingham City na West
Ham ambako pia bado alishindwa kuonyesha uwezo.
Bentley alikuwa
nje ya uwanja kwa miezi sita kufuatia kuwa na majeraha kule Upton Park, baada ya
kufanyiwa upasuaji wa mguu, hata hivyo alitarajiwa kurejea katika fomu akiwa Tottenham
baada ya kuwasili kwa Andre Villas-Boas, jambo ambalo pia aligonga mwamba.
Kinda huyo
wa zamani wa Arsenal ambaye kwa mara ya
mwisho kuitumikia timu ya taifa lake la Uingereza ilikuwa ni mwaka 2008, anaamini
kuwa bado anaweza kuichezea timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuachwa katika uteuzi wa hivi
karibuni wa meneja wa timu ya Taifa Roy Hodgson.
“nilidhani
meneja mpya angenipa nafasi, lakini inaonekana tayari kuna maji mengi chini ya
daraja"
Meireles:Nilikuwa na wakati mzuri
sana Chelsea nitaikumbuka sana klabu hii
Raul
Meireles amerejea katika viunga vya uwanja wake wa zamani wa klabu ya Chelsea vya Cobham hapo jana na kusema alikuwa katika kipindi kizuri cha maisha yake
alipokuwa hapo kabla ya kuondoka na kujiunga na klabu yake mpya ya Fenerbahce.
Kiungo huyo alipokuwa
katika kipindi cha utumishi wake wa miezi 12 Stanford Bridge, aliicheza Chelsea jumla ya michezo
48 ambapo alifanikiwa kushinda mataji ya mawili ya FA na ligi ya mabingwa ulaya
Kiungo huyo
alikosekana katika mchezo wa fainali ya mabingwa kufuatia kupewa kadi nyekundu
kule Camp Nou katika mchezo wa nusu fainali ya pili lakini bado alipata medali
, ambayo kwake imekuwa ni fahari ya maisha yake ndani ya Stanford Bridge maeneo ya London
ya kaskazini.
Amenukuliwa kupitia
mtandao wa Chelsea akisema
"nimekuja
kuwaaga marafiki zangu na kwa kweli nitaikumbuka klabu hii, mashabiki wake na
jiji pia"
"kuna
watu wazuri hapa ambao walinipa nguvu na wanasaidia kila mtu , hivyo nimekuja
kuwaaga wote."
Meireles alijiungana
Chelsea kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni €15 akitokea Liverpool.
Casillas anasema anataka kukaa miaka
minane zaidi Madrid
Mlinda mlango
wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas amethibitisha kuwa
mpango wake ni kuendelea kusalia katika klabu yake hiyo na kumalizia soka yake
hapo, klabu ambayo alijiunga nayo akitokea kituo cha kukuza vijana cha Castilla.
Mlinda mlango
huyo mwenye umri wa miaka 31 alianza kuidakia klabu hiyo akiwa na umri wa miaka
18 na katika maadhimisho yake ya kuwepo katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka
13, amenukuliwa akisema hana mpango wa kuondoka mpaka atakapo staafu kucheza
soka.
“Ndoto yangu itakuwa kweli kama nitamalizia soka langu hapa".
"nilikuwa
na ndoto ya kuichezea klabu hii tangu nikiwa na umri wa miaka minane , muda
unakwenda haraka lakini nafurahia sana kile ambacho Real Madrid inanipatia na
kile ambacho mimi pia nakitoa katika klabu."
Tangu ajiunge
na Madrid , Casillas amekusanya mataji mbalimbali yakiwemo mataji mawili ya
ligi ya mabingwa ulaya , mawili ya Intercontinental Cups,matano ya ligi, moja
la Copa del Rey, moja la European Super
Cup na matatu ya Spanish Supercopas.
Pia
ameshinda mataji ya kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya akiwa na timu
ya taifa ya Hispania.
Ameendelea kusema
kuwa
"miaka
13 imekwenda lakini tegemea mengi mazuri toka kwangu,".
"mkataba
wangu unamalizika mpakara nitakapo kuwa na umri wa miaka 36, na ndoto yangu ni kustaafu nitakapo fikisha umri wa miaka
39”
Brazil kucheza na England kuadhimisha miaka 150 ya kuzaliwa kwa chama cha soka cha England FA.
Timu ya
taifa ya Uingereza inatarajia kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Brazil katika
uwanja wa Wembley ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki kuadhimisha miaka 150
ya chama cha soka cha Uingereza FA.
FA
imetangaza kuwa mabingwa mara tano wa kombe la dunia watacheza na kikosi cha
meneja Roy Hodgson Jumatano ya February 6 mwakani , pia kucheza na Brazil katika
mchezo wa pili wa marudiano katika kipindi cha kiangazi.
Mchezo mwingine
wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland, umepangwa kuchezwa katika dimba jipya la Wembley, May 29, wakati ambapo jirani Scotland wakipangiwa kucheza mwezi August.
No comments:
Post a Comment