KOCHA Mkuu wa Yanga,
Tom Saintfiet ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya
ufunguzi ya michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons
itakayochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam hii leo,
Saintfiet amesema ameteua wachezaji hao kutokana na mazingira ya mechi hiyo na
pia uwezo waliouonyesha katika mechi za hivi karibuni za kirafiki na michuano ya Kombe la
Kagame.
Amewataja wachezaji wanaotarajiwa kuondoka kesho asubuhi
kwenda Mbeya kuwa ni walinda mlango Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Shadrack
Nsajigwa, Juma abdul, Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, David Luhende,
Oscar Joshua na Stefano Mwasyika.
Viungo kuwa ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna
Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nizar Khalfan, Shamte Ally na Simon
Msuva wakati washambuliaji ni Jerry Tegete, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na
Hamisi Kiiza.
Wachezaji ambao hawatakuwepo safarini Mbeya kwa ajili ya mechi hiyo kuwa ni kipa Said Mohamed, Ladislaus Mbogo, Job
Ibrahim, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin Bakari, Idrisa
Assega na Issa Ngao wa Yanga B, ambaye anakomazwa kikosi cha kwanza.
Pia kocha
huyo amesema mchezo wao dhidi ya Prisons utakuwa mgumu kwa
vile wapinzani wao watakuwa wakicheza kwenye uwanja wa nyumbani na mbele ya
mashabiki wao, hivyo amejipanga vyema kukabiliana nao ili aweze kutimiza lengo la
kuibuka na ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo
No comments:
Post a Comment