KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 30, 2012

FELIPE SCOLARI KUONGOZA BRAZIL FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA. MTIHANI WAKE WA KWANZA DHIDI YA ENGLAND FEBRUARI.



Luiz Felipe Scolari amethibitishwa kuwa meneja mpya wa timu ya taifa ya Brazil kufuatia kuondolewa mtangulizi wake Mano Menezes wiki iliyopita.

Taarifa zilizokuwa zimezagaa tangu jumatano zilikuwa zinaashiria  Scolari kupewa nafasi hiyo na jana shirikisho la soka la Brazil likamthibitisha kurejea kukiongoza kikosi cha timu ya timu ya taifa ya Brazil.

Scolari aliiongoza Brazil mpaka kunyakua taji la kombe la dunia mwaka 2002 na atakuwa kiongozi wa benchi la ufundi la mabingwa hao mara tano wa kombe la dunia kwenye fainali za mwaka 2014 ambalo Brazil ndio wenyeji.

Bosi huyo wa zamani wa Chelsea alikuwa nje ya kazi tangu alipoachana na Palmeiras mwezi September, ambapo kabla ya alikuwa akikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Ureno katika fainali za kombe la duna za mwaka 2006 na mwaka 2004 na 2008 michuano ya Ulaya.

Amenukuliwa baada ya uteuzi wake akisema
"najisikia raha na kuwa tayari,  najihisi kijana , najihisi naweza, tunalazimika kushinda taji, kwasasa hatuonekani kama tunauwezo huo lakini tunapaswa kuwepo katika wale wanaotajwa kushinda taji. Kuwa katika nafasi ya tatu au nne si kitu kizuri kwa nchi ambayo imechukuwa taji hilo mara tano.

"sijihisi kuwa kwenye shinikizo najisikia furaha. Wakati Rais wa FA Marinaliponiita jumanne na kuthibitisha nimechaguliwa nilimshukuru kwa zaidi ya mara elfu moja.

"nilikuwa kwenye presha nilikuwa kwa mara ya kwanza tulipokuwa katika hatari ya kutokwenda kwenye fainali ya kombe la dunia''.

Pep Guardiola alikuwa kwenye orodha ya watu ambao walipewa nafasi katika kazi hiyo lakini Rais wa FA ya Brazil Jose Maria Marin ameweka wazi kuwa sifa kuu iliyompa kazi Scolari ni mafanikio yake katika ngazi ya kimataifa.

Atakuwa akisaidiwa na kocha mwingine aliyewahi kushinda kombe la dunia Carlos Alberto Parreira, ambaye aliiongoza Brazil mwaka 1994 kwenye fainali za nchini Marekani na sasa anarejea kama meneja.

Marin amenukuliwa akisema,
 "Baada ya kuchambua na kufikiria kwa muda mrefu ni akiina nani watakuwa bora katika soka la Brazil, kwa mashabiki wa Brazil, tuna mkabidhi jukumu la timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya ‘Confederations’ majira ya kiangazi na kombe la dunia, hivyo tuliona watu ambao walipata mafanikio mara mbili na ambao wanaheshimika kote duniani , ni Felipe and Parreira.''

Mchezo wa kwanza wa Scolari akiwa kocha mpya itakuwa ni dhidi yEngland katika uwanja wa Wembley utakao pigwa februari 6.

No comments:

Post a Comment