KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 13, 2012

KIINGILIO SERENGETI BOYS NA CONGO BRAZZAVILLE BUKU, UNATAKA NINI TENA.

Shirikisho la soka nchini TFF hii leo limetangaza viiingilio vya mchezo wa kuwania kufuvu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana kati ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys dhidi ya vijana wenzao kutoka Congo Brazzaville.

Akitangaza viingilio hivyo hii leo katibu wa TFF Angetille Oseah amesema kuwa ili kuhakikisha wadau wengi wa soka wanaelekea uwanja wa Taifa siku ya mchezo wameamua kama TFF kufanya eneo la VIP A kiingilio chake kuwa shiling elfu 5,000/-, VIP B kiingilio kitakuwa shilingi 2,000/- ilihali eneo lingine lote lilisalia kiingilio kitakuwa shilingi elfu 1,000/-.

Amesema ni vema watanzania wanawake kwa wanaume kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuipa nguvu timu hiyo ambayo mazingira ya kimaandalizi yanaonekana kuwa mazuri kwa maana ya eneo la ufundi kilichobaki ni ndani ya uwanja ambapo ni watanzania wenyewe sasa kusaidia katika kuishangilia kwa nguvu zote.

Viingilio vimependekezwa na kamati iliyoundwa hivi karibuni na Rais wa TFF leordigar Tenga ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo aliteuliwa Ridhiwani Kikwete.

Serengeti Boys imecheza michezo 15 na haijapoteza mchezo hata mmoja na hizo zikiwa ni salam kwa Congo Brazaville

No comments:

Post a Comment