Kiungo wa kimataifa wa Kenya na
Celtic ya Scoitland Victor Wanyama ameshindwa kuja nchini Tanzania na kikosi
cha timu yake ya Taifa ya Kenya Harambee Stars kutokana na kile kilichoelezwa
kuwa Shirikisho la soka la Kenya Kushindwa kutimiza masharti yake.
Wanyama hapo kabla aliitaka FKF kumrudishia
fidia ya nauli yake ya kurudia nchini Scotland ambapo inaarifiwa kuwa ilikuwa ni shilingi za
Kenya laki 325,000 (USD 3,200) ambazo zilitokana na mchezo wa oktoba 16 ambapo Wanyama alirejea
nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa Harambee Stars dhidi ya Afrika kusini FKF.
Fedha hizo hazikuweza kurejeshwa jambo ambalo halijatekelezwa mpaka
leo.
Imeelezwa kuwa familia ya Wanyama
imepinga kitendo kama hicho kujirudia wakitaka kwanza kuhakikishiwa juu ya
fedha hizo ambapo FKF imetaka kuzirejesha baada ya mchezo na Tanzania.
Amenukuliwa mama yake Wanyama Mildred
Ayiemba aking’aka
"hii FA ya Kenya inacheza na
mwanagu"
"Victor alipowauliza juu ya pesa yake maafisa wa FA walikuwa wanamzungusha
wachezaji wote wanapewa tiketi za kurudia kwanini hivyo kwa mwanangu?"
Harambee Stars iliwasili jijini Mwanza tangu jana
usiku majira ya saa nne bila ya wachezaji wake wawili tegemeo Victor
Wanyama na Arnold Orig Otieno huku FKF ikishindwa kuieleza TFF sababu za wachezaji kutokufika.
Wachezaji walio wasili ni pamoja na Dennis Oliech, Ayub
Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos), Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko
Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC
Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).
Wengine ni Geofrey Kokoyo
Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma
(Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba, Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew
Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.
Viongozi ni kocha Henry Louis
Michel akisaidiwa na Mohammed Ajam Boujarari, Florent Louis Robert Motta, Sunil
Shah, Wycliff Obiero Makanga, Wilberforce Bruce Juma, Benson Kennedy Otieno,
Ali Abdallah Rehan, Robert Asembo Akumu na Angeline Mwikali Nzavi.
No comments:
Post a Comment