Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) limeamua
kurudisha nyuma pambano la watani wa jadi katika soka la nchini Kenya baina ya Gor
Mahia na AFC Leopards pambano ambalo ni la michuano ya FKF ambapo sasa pambano hilo
litapigwa Jumamosi badala ya jumapili.
Katika mkutano uliohudhuriwa na maafisa
wa vilabu vyote viwili Gor Mahia na AFC Leopards na kusimamiwa na Rais wa FA
Sam Nyamweya kimsingi wamekubaliano mchezo huo upigwe jumamosi katika dimba la Kasarani.
Huo ni mchezo wa nusu fainali ambapo
nusu fainali nyingine itakuwa ni kati ya Sofapaka dhidi ya mabingwa wapya wa
taji la ligi kuu nchini humo Tusker FC, mchezo ambao utapigwa jumapili huko City
Stadium.
Licha ya kuendelea kusugua benchi Balotelli hana mpango wa kuiacha Manchester
City.
Wakala wa mshambuliaji Mario Balotelli, Mino
Raiola amekaririwa akisema kuwa mshambuliaji huyo hana nia ya kuihama klabu yake
ya Manchester City, licha ya kuwepo taarifa kuwa mshambuliaji huyo amekuwa
akisaka timu ambayo atapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza
Maneno hayo ya wakala huyo yanafuatia
baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia kutokuwepo katika kikosi
kilichocheza dhidi ya Tottenham jumapili ambapo pia hakuwepo hata katika orodha
ya wachezaji wa akiba.
Katika wiki za hivi karibuni Sergio
Aguero na Carlos Tevez wamekuwa wakiwakilisha kikosi cha meneja Roberto Mancini
wakati ambapo Edin Dzeko amekuwa akiingizwa akitokea katika benchi.
Raiola anasema
"Baloteli hana mpango wa kuondoka"
DECO :Neymar ni kundi moja na akina Messi
na Ronaldo.
Kiungo wa zamani wa Barcelona Deco amewapongeza
washambuliaji Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, lakini pia anadhani pia
mshambuliaji wa Santos Neymar anastahili kuwemo katika kundi moja na
washambuliaji hao.
No comments:
Post a Comment