Stars ikiwa mazoezini Kirumba jana asubuhi ikiwa ni maandalizi ya mechi ya leo. Stars inadhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager.
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars chini ya kocha wake raia wa Dernmark Kim Poulsen hii leo inashuka katika dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.
Huu ni mchezo unaochezwa katika kalenda inayotambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA ambapo mataifa mbalimbali hutumia tarehe za michezo ya kalenda ya FIFA kujaribu kupandisha madaraja nchi zao katika viwango vya ubora vya FIFA endapo wataibuka na ushindi.
Stars itakuwa ikiwategemea zaidi washambuliaji wake Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa, John Bocco, Simon Msuva na Edward Christopher kuhakikisha wanaibomoa ngome ya Harambee Stars huku sehemu ya kiungo ikitarajiwa kuwatumia Athumani Iddi Chuji, Shabani Nditi, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Ramadhani Singano Mwinyi kazimoto na Frank Domayo.
Ngome ya Stars itakuwa ikiwategemea
Nassor Masoud, Agrey Morris, Kelvin Yondani, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Amir Maftah and Issa Rashid .
Nassor Masoud, Agrey Morris, Kelvin Yondani, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Amir Maftah and Issa Rashid .
Walinda mlango ni Juma Kaseja na Deogratius Munish Dida.
Jana mdhamini wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager aliwataka
wachezaji wa timu ya taifa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kimchezo na kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi hiyo ya jioni ya leo.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, alisema wao kama wadhamini wana imani na timu ya taifa na Kocha wake Kim Poulsen.
Kavishe aliendelea kusema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha TFF kuipeleka
timu Mwanza kucheza mechi ya kirafikii dhidi ya Kenya na pia kujiandaa na
mashindano ya CECAFA Challenge yanayotarajia kuanza Jijini kampala tarehe 24
mwezi huu.
Tangu Stars ipate mdhamini mpya, Kilimanjaro Premium Lager, imeshacheza dhidi ya Ivory Coast, Msumbiji, Botswana na Namibia Kilimanjaro Premium Lager imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni mbili kuidhamini Taifa Stars kwa miaka mitano ijayo.
Yenyewe Harambee Stars itakosa huduma ya kiungo wake Victor Wanyama anaechezea klabu ya Celtic ya Scotland kutoka na kiungo huyo kuwa na matatizo na uongozi wa soka nchini Kenya FKF sababu ambazo zinaonekana kuwa ni za kimaslahi zaidi.
Wanyama amekuwa akilidai shirikisho la soka la nchini Kenya fedha za nauli ya kwenda na kurudi nchini Kenya akitokea katika klabu yake.
Pia Harambee Stars itamkosa mlinda mlango wake nambari moja Arnod Orig ambo nafasi zao zimezibwa na mlinda mlango wa Ulinzi Jactone Odhiambo na kiungo wa Gor Mahia Antony Akumu.
Huu ni mchezo wa pili kwa kocha wa Harambee Stars, Henri Michel ambapo mchezo wa kwanza dhidi ya Afrika Kusini timu hiyo ilichapwa mabao 2-1 jijini Nairobi mwezi Oktoba.
Kikosi cha Harambee Stars kikifanyishwa mazoezi na kocha wake Henri Michel
Harambee Stars itawatumia Dennis Oliech(nahodha), Ayub
Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos), Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko
Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC
Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).
Wengine ni Geofrey Kokoyo
Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma
(Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba, Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew
Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.
No comments:
Post a Comment