Steven Gerrard anasema hana muda na kauli ya Rio Ferdinand (pichani chini) aliyesema England imepoteza utambulisho wake.
Steven Gerrard amejibu kauli iliyotolewa na mkongwe mwenzake Rio Ferdinand aliyedai kuwa England haina utambulisho na kwamba mfumo unaotumika ni wa kunakili.
Ferdinand Jumatatu alifunguka waziwazi kwa kusema kuwa hakuna daraja linalo unganisha timu ya vijana na timu ya wakubwa na hiyo itapelekea taifa hilo kushindwa kufuzu katika mashindano mengi ya kimataifa yajao kutokana na kuiga mifumo ya wengine ya kulazimisha.
Hata hivyo nahodha wa timu ya taifa ya England Steven Gerrard, amezungumzia hilo muda mfupi kuelekea katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Scotland utakao pigwa muda mfupi ujao katika dimba la Wembley kwa kukanusha shutumu hizo.
‘Sina muda na kufikiri kile kilichosemwa na Rio kuhusu makundi ya wachezaji.
‘Unapoichezea England, kwa kawaida kunakuwa na maoni mengi kutoka nje ya timu hususani katika kipindi cha mwaka wa kombe la dunia.
‘Kutakuwa na maoni ya watu wengi lakini unapokuwa ndani unapiokuwa ndani huwezi kuchukua kile kinachosemwa na watu wa nje.
‘Timu hii ina utambulisho wake na tuna nzuri, baadhi ni wachezaji wakubwa na nina imani tutadhihirisha hilo mwaka huu.’
Gerrard na Wayne Rooney (katikati) akiongoza England katika mazoezi huko St. George's Park.
Gerrard (kulia) na Rooney wakivuta wakiafanya mazoezi.
Ferdinand alidai kuwa meneja wa timun ya taifa ya England ananakili utambulisho wa Glenn Hoddle, ambaye alimchukua yeye kutoka katika West Ham akiwa kinda katika mfumo uliotumiwa katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1998.
Ferdinand alipokuwa kinda alicheza na wakongwe kama Paul Gascoigne (Gaza) chini ya Glenn Hoddle (pichani chini)
Glenn Hoddle na Rio Ferdinand mwaka 1997.
‘Kuna mfumo mpya unawekwa pale St George’s Park .Tulianza kuliona pale Glenn Hoddle alipokuwa meneja , kiasi kulikuwa na utambulisho wa kuingia na kutoka kwa football.
‘Tangu wakati wakati huo sidhani kama kuna utambulisho halisi. Kama majina yote yameondolewa mgongoni na rangi kubadilishwa huwezi kusema ni timu ya England.
‘Inonekana kama timu ya taifa ya Italia, Uholanzi, Hispania, Ujrumani au Brazil, Bila kuona majina ya wachezaji huwezi kujua kwani wanafanya kazi kupitia karatasi.
No comments:
Post a Comment