Pele apata nafuu baada ya kufanyiwa
upasuaji wa nyonga.
Nyota wa
zamani wa klabu ya Santos na timu ya taifa ya Brazil ambaye pia ni alama muhimu
katika ulimwengu wa soka Edison Arantes do Nascimento ‘Pele’ amefanyiwa
upasuaji wa nyonga na inaarifiwa ya kwamba anaendelea vizuri baada ya kuwa
katika uangalizi mzuri mjini Sao Paulo.
Pele ambaye
kwasasa ana umri wa miaka 72, alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Albert
Einstein licha ya kwamba hakuna habari zaidi zilizo tolewa ikiwa ni agizo kutoka
kwa familia ya gwiji huyo wa soka wa zamani.
Msemaji wake
Jose Fornos ameidokeza Agence France-Presse akisema;
"kila
kitu kimekwenda vizuri na ulikuwa ni upasuaji mdogo"
Pele anaangaliwa
kama ni mchezaji mkubwa kuwahi kutokea duniani akifunga magoli 1,300 na
kushinda mataji matatu ya kombe la dunia katika miaka ya 1958, 1962 na 1970
katika cha uchezaji wake ulio tukuka.
Baada ya
kuendelea kushikilia rekodi nyingi za dunia katika soka, hatimaye Pele wiki
iliyopita alishuhudia moja ya rekodi yake ikivunjwa na mshambuliaji wa
kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi ya kufunga magoli 75 katika
kipindi cha mwaka mmoja
Evra: Itadhihirisha kushindwa kwangu
katika soka endapo sitapata taji lolote na timu ya taifa ya Ufaransa
Mlinzi wa Manchester
United na timu ya taifa ya Ufaransa Patrice Evra amesema waziwazi kuwa itakuwa
ni sawa na kukosa mafanikio katika maisha yake ya soka endapo atakosa taji akiwa kama mchezaji wa timu ya taifa
ya nchi yake ya Ufaransa.
Mlinzi huyo wa
pembeni wa zamani wa Monaco alianza kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa ‘Les
Bleus’ mwaka 2004 na tangu wakati huo amesha ichezea jumla ya michezo 46 akiwakilisha
katika michuano mikubwa minne pamoja na kuwa nahodha wa kikosi hicho katika
fainali za kombe la dunia mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini.
Mlinzi huyo
mzaliwa wa Senegal anaamini kikosi cha Ufaransa kwasasa kinasukwa vizuri
na kocha Didier Deschamps na kimeanza kuimarika, licha ya matatizo kadhaa kuendelea kuzonga soka la Ufaransa.
Akiongea na
gaeti la kifaransa la Gazzetta Dello Sport amesema,
"Baada
ya kombe la dunia 2010, Italia imeimarisha namna ya uchezaji wao lakini
Ufaransa bado kuna matatizo"
"nataka
kushinda nikiwa na timu ya taifa, itakuwa ni kushindwa endapo nitashindwa
kupata taji "
"chini
ya Blanc nilipoteza nafasi yangu ya kudumu lakini sasa chini ya Deschamps mambo
yamekuwa mazuri. Kocha ameniambia kama nitacheza vizuri nitakupa nafasi ya kudumu.'"
Ufaransa itashuka
dimbani dhidi ya Italia katika dimba la Stadio Ennio Tardini mjini Parma usiku huu katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Wilfried Bony kujiunga na Chelsea Januari.
Mshambuliaji
wa Vitesse Wilfried Bony amekaribisha tetesi juu ya klabu ya Chelsea kutaka
huduma yake katika kipindi cha uhamisho cha mwezi January.
Bony mwenye
umri wa miaka 23, amekuwa katika kiwango huko Eredivisie tangu kuihama klabu
yake ya zamani ya Sparta Prague mwezi January 2011, akiwa amesha pachika wavuni
jumla ya mabao 12 baada ya kushuka dimbani mara 11 katika msimu huu.
Mapema mwezi
huu wakala wa mchezaji huyo Francis Kacou alinukuliwa akisema,
"kuna
vilabu kadhaa vya ligi kuu nchini England vimeonyesha nia ikiwemo Chelsea na
Aston Villa"
Katika mahojiano
yake na jarida moja la nchini Czech la Pravo, nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alithibitisha
kuwa angependelea kuelekea Stamford Bridge.
"sitaki
kuongea mengi kuhusu hilo lakini kama imeandikwa kuwa nakwenda huko basi ni
kitu kizuri"
"kama wananitaka nitakuwa ni heshima
kubwa. Napenda kujiunga na klabu kama hiyo, napenda soka na England na siogopi
kwenda huko. Chelsea ni klabu kubwa"
Mkurugenzi wa
michezo wa Chelsea Michael Emenalo hivi karibini alielekea Arnhem kuangalia
mchezo baina ya Vitesse dhidi ya FC
Twente ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0.
Santos imethibitisha kumtaka Robinho.
Kocha wa Santos
Muricy Ramalho ameweka wazi kuwa klabu yake ina matumaini makubwa ya kumrejesha
mshambuliaji wa AC Milan Robinho katika uhamisho wa mwezi Januari.
Taarifa kutoka
nchini Brazil zimedai Robinho, Nene, Pablo Aimar na Diego ni miongoni mwa
wachezaji walio katika orodha ya kocha Ramalho kwa ajili ya msimu ujao wakati
ambapo kuna tetesi kuwa huenda klabu hiyo ikampoteza mshambuliaji wake hodari Felipe
Anderson.
Mapema wiki
hii alikaririwa mwanasheria wa Robinho Marisa Alija akisema Robinho ana
matumaini ya kurudi Santos, lakini alikataa kusema itakuwa lini.
"tunasikia
mengi juu ya Robinho lakini tukumbuke ana mkataba na Milan mpaka 2014,"
"hajaniambia chochote juu ya kurejea Santos
msimu ujao. Lakini anashindwa kuficha juu ya nia yake ya kurejea lakini katika
hatua hii sidhani kama itawezekana."
Ibrahimovic anataka Steven Gerrard ondoke England
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic anaamini wakati umefika sasa kwa kiungo
mzoefu wa Liverpool Steven Gerrard kuondoka katika soka na England na kujiunga
na vilabu vingine vikubwa nje ya nchi yake.
Ibrahimovic ametoka
maoni yake hayo wakati huu ambapo Sweden inaelekea kucheza na timu ya taifa ya
England maarufu kama Simba watatu mjini Stockholm ukiwa ni mchezo wa kimataifa
wa kirafiki.
Muda mfupi baada
ya mchezo wao akiwa na klabu yake ya Paris Saint-Germain dhidi ya Liverpool Zlatan
alionyesha wazi kumkubali Gerrard, lakini akasema ni muda muafaka kwa Skipper
huyo kuondoka Premier League.
"nadhani
Steven Gerrard anaheshimika kote barani ulaya, nafahamu hilo kwasababu mara nyingi kocha huwa
anasema kuwa muangalifu na Gerrard kwasababu ndiyo mchezaji anaye leta utofauti
uwanjani.
"lakini
licha ya Liverpool kuwa klabu kubwa Ulaya, ningependa kumuona Steven katika klabu
nyingine kubwa Ulaya.
"kwangu
mimi mchezaji mzuri ni yule anaye onyesha utofauti kila sehemu. Nina uhakika Steven
Gerrard anaweza."
No comments:
Post a Comment