KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 14, 2012

WAKATI YANGA IKIENDA MAPUMZIKO YA WIKI MBILI , DIDIER KAVUMBAGU ANAONGOZA KWA MAGOLI SAWA NA TCHECHE

Kikosi cha Young Africans Sports Club
Uongozi wa klabu ya Young Africans umewapa mapumziko ya wiki mbili wachezaji wake wote kufuatia kuwepo kwa mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyomalizika mwishoni mwa wiki na kuendelea tena mwakani mwezi Januari 2013.
Kocha Mkuu Ernest Brandsts amesema wameamua kutoa mapumziko hayo kufuatia wachezaji hao kuwa na timu tangu mwezi wa nane wakati wa maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom hivyo hawajapata nafasi ya kupumzika na familia zao.
Young Africans imemaliza mzunguko wa kwanza kwa kufikisha pointi 19, kufuatia kucheza michezo 13, imeshinda michezo 8, imetoka sare michezo 2 na kufungwa michezo 2, aidha pia imefunga mabao 25 na kufungwa mabao 10.
Mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Young Africans anaongoza kwa kufunga mbao 8 sambamba na mchezaji Kipre Tchetche wa timu ya Azam. 
Wachezaji Kelvin Yondani, Frank Domayo, Saimon msuva na Athumani Idd 'Chuji, wamejiunga na timu ya Taifa ya Tannzania 'Taifa Stars' ambayo inacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars katika mchezo huo uliopo katika kalenda za FIFA.
Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite,Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wanatarajiwa kujiunga na timu zao za Taifa katikati ya wiki hii, kwa ajili ya maandalizi ya  mashindano la TUSKER CECAFA Cup ambayo mwaka huu yatafanyika nchini Uganda kuanzia Novemba 24.
Wachezaji wote waliobakia ambao hawatajiunga na timu zao za Taifa watarejea klabu tarehe 26 Novemba tayari kwa kuanza mazoezi tarehe 27 Novemba ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu. 

No comments:

Post a Comment